Lakini sio kama makosa ya herufi katika kombe kubwa la soka, hii imetokea Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Siku ya Jumatano usiku klabu ya Simba iliwalaza wapinzani wao wa jadi Yanga kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya kombe la kufungua msimu la Community Shield.

Lakini ni mashabiki waangalifu walioona makosa ya herufi katika maandishi ya kombe hilo.

Neno Shield liliandikwa kimakosa na kusomeka ''Sheild'' lakini hilo halikusitisha sherehe za kulikabidhi kwa mshindi kombe hilo.

Hata hivyo tayari chama cha Soka nchini Tanzania kimewataka radhi mashabiki wa soka na wameiomba timu ya Simba kurejesha ngao hiyo ili iweze kufanyiwa marekebisho haraka.

 


Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top