Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, hakuna
kitakayempitisha kugombea urais 2015, kwa presha za makundi au wapambe.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika vyumba vya
habari mbalimbali jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema,
mfumo wa CCM katika kuwapata wagombea ni imara kiasi kwamba hautaweza
kuathiriwa na presha za makundi wakati wa kuteua mgombea urais katika uchaguzi
mkuu mwaka huu.
Amesema, ni vigezo vinavyozingatia kanuni na katiba ya
Chama tu ndivyo vitakavyomuwezesha anayetaka kupeperusha bendera ya CCM
kupitishwa na Chama, vinginevyo haitawezekana hata kama ana makundi yenye
presha kiasi gani.
"Chama hiki kina mfumo na taratibu ambazo
haziwezi kusukumwa na presha za wapambe wa mgombea yeyote, na hata kumbukumbu
zinaonyesha kwamba katika chaguzi zilizopita, wamewahi kuwepo wagombea wenye
makundi yenye presha kiasi cha kudhaniwa ndio wangeteuliwa, lakini baada ya
kufika mbele ya taratibu na kanuni waliachwa na nafasi kupewa wengine",
alisema Nape.
Alisema, kanuni na taratibu ndizo mwamuzi wa mwisho
katika kuteua wagombea wa CCM, "Sisi tukisema wanaotaka nafasi hii njooni
mjipime hapa, mmojawapo akijaiona hatoshi lakini kwa ujanja akaongeza matofali
kupata urefu... huyo taratibu zitatumia kuondoa matofali ili abaki kama alivyo
kuona kama anatosha", alisema Nape.
"Na katika
utaratibu huu wa kuondoa matofali ndiyo watajitokeza baadhi yao kulalamika kwa
sababu itauma kidogo", alisema.
From: mitandao ya kijamii!
From: mitandao ya kijamii!
Post a Comment