Maneno haya machache yamenakiliwa kutoka Gazeti la Mwananchi, ambayo yalitamkwa na mwanasheria mkuu wa serikali nchini, George Masaju alipozungumza na uongozi wa gazeti hilo hivi karibuni.
Ki ukweli Madhehebu yote ya dini nchini ukiachilia mbali Uislamu yana taasisi zake mbalimbali na zote zimesajiliwa na zinatambuliwa na serikali, leo mwanasheria kudai serikali inaitambua BAKWATA peke yake, ni wazi taasisi nyingine zilipatiwa usajili FEKIIII!! Soma mwenyewe alivyofafanua siku hiyo:-
"Kuhusu kugawanyika kwa Waislamu katika kulitambua Baraza la Waislamu
Tanzania (BAKWATA), Masaju alisema hakuna jinsi ya kulikwepa baraza hilo kwa
kuwa ni chombo kinachotambuliwa na Serikali kisheria.
“Kwanza kwa mfumo wetu wa sheria, taasisi ile ya BAKWATA ndio inayotambulika
kabisa kisheria, hivyo endapo wapo wanaoipenda au wasioitaka, hakuna jinsi ya
kuikwepa” alisema.
Lakini akasema kuwa katika suala hilo, Waislamu wote waliungana na kuwa na
msimamo mmoja.
“Na sisi tunacholenga kama serikali ni kuhakikisha kuwa watu wote katika
jamii wanakuwa na amani,” alisema.
Alisema kuwa walikutana na viongozi hao wa Kiislamu Februari 3 na walikiri
kuwapo na tofauti, lakini wakasema tofauti walizokuwa nazo wameziondoa na
wameungana kutokana na umuhimu wa kuwapo kwa mahakama hiyo.
Post a Comment