Je wajua kwamba mbu huvutiwa na vitu vitamu?.
Hivyobasi wanasayansi wametumia fursa hiyo
kutengeza dawa iliochanganywa na sukari ili kuwavutia kwa lengo la kuwaua.
Dawa hiyo imechanganywa na kemikali iliowekwa
harufu ya sukari inayoweza kuwavutia wadudu hao .
Imegunduliwa kuweza kuangamiza mbu katika
vijiji vya Tanzania vyenye ugonjwa mwingi wa malaria ambapo majaribio
yamefanywa.
Dawa hiyo kwa jina Vectrax inaweza kupiga jeki
juhudi za kupunguza malaria, Zika na magonjwa mengine yanayosababishwa na mbu
duniani.
Mwanasayansi wa Brazil aliyenzisha dawa hiyo
Agenor Mafra Neto anasema kuwa lengo lake ni kuifanya kuwa ya bei rahisi na
kuhakikisha kuwa imesambazwa kupitia Umoja wa Mataifa na mashirika yasiokuwa ya
kiserikali.
"Mchanganyiko wa kemikali tunayotumia
kuwavutia mbu una nguvu mno hatua ambayo inawafanya kutovutiwa na harufu
nyengine za mimea ya kawaida'', alisema Agenor.
Anasema kuwa ni sawa na kuwa na duka la
chocolate katika kila pembe.
Bidhaa hiyo ni kivutio kikubwa hatua
inayowafanya kuila licha ya kuwa na kemikali za dawa ya wadudu.
Mbali na hilo mabaki ya dawa hiyo yanaweza
kuchafua udongo na kuukinga dhidi ya wadudu.Kwa kutengeza dawa hiyo wanasayansi
hao walitumia harufu ya maua na mimea mingine inayotoa nekta .
Baadaye walitumia gesi ya
chromatography-electroantennographic (GC-EAD) kutenga na kubaini vitu vyenye
harufu mbaya ndani yake.
Waliweka antena za wadudu hao katika maelfu ya
vitu hivyo kubaini ni vipi vinaweza kuwa na athari ya kibaiolojia.
Waliondoa harufu zozote ambazo zinaweza
kuwavutia nyuki.
Baadaye walitumia mchanganyinko wa kemikali
wenye sukari na protini kuigiza kemikali 20 zinazoweza kuwavutia mbu katika
maua yanayotoa nekta na kuwashawishi kula.
Mchanganyiko maalum wa kemikali hizo na dawa ya
wadudu kama vile pyrethroids ama spinosad ulitengeza dawa yenye nguvu.
Watafiti hao kwa sasa wanafanya utafiti nchini
Tanzania ,ambapo asilimia 93 ya raia wako hatarini kuambukizwa magonjwa ya
malaria.
Katika matokeo yao walibaini kwamba idadi ya
mbu ilipungua kwa thuluthi mbili katika muda wa wiki mbili miongoni mwa jamii zilizotibiwa
na Vetrax ikilinganishwa na zile ambazo hazikutibiwa na dawa hiyo.
''Iwapo hali itaendelea ilivyo, tunataraji
kwamba idadi ya mbu wanaosambaza malaria itaangamia kabisa katika maeneo ya
vijiji vilivyotibiwa'', alisema Mafra-Neto.
Ana matumaini ya kuwa na data zaidi kutokana na
utafiti huo hivi karibuni.
Huku Mafra Neto akitambua kwamba mbu huwa na
jukumu dogo katika chakula kupitia kuwasaidia wanyama wadogo kama vile samaki
na buibui, angependelea kuwaona wachache hususan katika mataifa yalio na
ugonjwa wa malaria.
Chanzo: BBC Swahili
Post a Comment