MKUU wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amelipongeza Shirika la Rafiki Social Development Organization – SDO la mkoani Shinyanga kwa kazi kubwa inayofanya ya kuwakomboa mabinti walioko katika makundi maalumu waliokuwa wakiishi katika mazingira hatarishi.
Pongezi
hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita katika sherehe za Siku ya Familia
kwa watumishi wa Shirika la Rafiki zilizofanyika eneo la Songwa Club wilayani
Kishapu mkoani Shinyanga ambapo mkuu huyo alikuwa mgeni rasmi.
Katika
sherehe hizo mkuu wa wilaya alikabidhi hundi ya shilingi milioni moja kwa moja
ya vikundi vya mabinti waliopo kwenye makundi maalumu kiitwacho “Wazawa” Mama
Lishe chenye makazi yake mjini Shinyanga.
Fedha
hizo zimetolewa na Shirika la Rafiki kupitia mradi wake wa SAUTI kwa lengo la
kusaidia kukuza mtaji wa kikundi hicho baada ya washiriki wake kuamua kuondoka
mitaani na kuamua kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali wakiendesha mgahawa wa kuuza vyakula.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Rafiki - SDO, Gerald Ng'ong'a. |
Akikabidhi
hundi hiyo, Matiro aliwataka walengwa wa kikundi hicho kutumia vizuri msaada
waliopatiwa na wakawe mabalozi wazuri kwa mabinti wengine ambao bado wako
mitaani wakiishi maisha ya dhiki kufanya vitendo visivyofaa mfano kudiriki
kuuza miili yao (dadapoa) ili na wao wabadilike kitabia.
Hata
hivyo alisema baadhi ya mabinti walioko mitaani hawafanyi wanayoyafana kwa
kupenda kwao bali wanasukumwa hali ngumu ya maisha waliyonayo na kwamba iwapo
wataelimishwa na kupewa ushauri mzuri wanaweza kubadilika kama baadhi yao
walivyobadilika na kuanza kufanya shughuli za uzalishajimali.
“Nawapongeza
wenzetu wa shirika la Rafiki kwa kazi nzuri wanayoifanya, binafsi nimekuwa
nikitembelea baadhi ya walengwa na kuona kweli hivi sasa wameamua kubadilika,
walisikiliza ushauri wangu, niliwaambia hakuna kisichowezekana iwapo wataamua
kuachana na vitendo visivyofaa,”
“Niwaombe
sana hakikisheni mnatumia vizuri msaada huu, uwe chachu ya maendeleo yenu,
nanyi wenyewe kaweni mabalozi wazuri kwa wengine, waone kumbe wakiamua
kubadilika wanaweza kuwa raia wema, na niwaombe ambao bado wanajihusisha na
vitendo vichafu waache sasa, wabadilikie, ikishindakana tutawafukuza,” alieleza
Matiro.
Wageni waalikwa na watumishi wa Shirika la Rafiki - SDO wakipongezana kwa kugonganisha grasi za vinywaji vyao na mgeni rasmi (Cheers). |
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akitoa hotuba yake. |
“Mkiendesha
shughuli zenu kwa kushirikiana mtaweza kujipanga nani afanye nini na mwingine
afanye kitu gani, hii itaondoa nyote kujikita katika uendeshaji wa miradi
inayofanana, mkifanya hivyo naamini mtaisaidia serikali yenu katika kuwapatia
maendeleo wananchi wake,” alieleza.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kikundi cha “Wazawa” Mama Lishe, Fatuma Jumanne
alimshukuru mkuu wa wilaya kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuwashawishi mabinti
waliokuwa mitaani waweze kujikusanya na kuunda vikundi vya uzalishaji mali.
Fatuma
alisema baadhi yao waliitikia wito wake ambapo pia walikutana na wawakilishi wa
Shirika la Rafiki lililoamua kuwachukua na kuwapatia mafunzo mbalimbali ikiwemo
yaliyohusu mabadiliko ya tabia na ujasiriamali na hivi sasa wameamua kuanzisha
shughuli za mama lishe.
“Kwa
kweli hatuna budi kukushuru sana mkuu wetu wa wilaya kwa juhudi zako
ulizozifanya za kutuhamasisha kujiunga kwenye kikundi hiki, tulisikiliza
ushauri wako na tumeanza kuona matunda yake, lakini pia tunawashukuru wafadhili
wetu shirika la Rafiki,”
“Wao
wamewahi kufanya kile ambacho ilikuwa kifanywe na serikali, wametupatia msaada
huu, tunaahidi kuutumia vizuri, na tutakuwa mfano mzuri kwa wenzetu wengine
ambao bado wako mitaani wakihangaika, na tunaomba msituchoke kila pale
tutakapohitaji msaada au ushauri wowote kutoka kwenu,” alieleza Fatuma.
Mkurugenzi wa Shirika la Rafiki - SDO, Gerald Ng'ong'a akitoa taarifa ya shughuli zinazotekelezwa na shirika mbele ya mgeni rasmi. |
Awali
katika taarifa yake kwa mgeni rasmi, mkurugenzi wa Shirika la Rafiki SDO,
Gerald Ng’ong’a alisema shirika lake kwa hivi sasa linaendesha miradi mitatu
inayotekelezwa katika manispaa ya Shinyanga, halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
na Kahama.
Ng’ong’a
aliitaja miradi inayotekelezwa na Shirika lake kuwa ni pamoja na mradi wa SAUTI
unaolenga kutoa elimu ya mabadiliko ya tabia na afya kwa makundi maalumu na
mabinti wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 24 ambao unatekelezwa manispaa ya
Shinyanga, kupiga vita mimba na ndoa za utotoni uliopo Kahama mjini.
“Mheshimiwa
mgeni rasmi, mradi mwingine ni ule wa Kuwaondoa watoto kwenye ajira mbaya
katika migodi midogo ya dhahabu iliyopo wilayani Kahama na kata ya Mwakitolyo
kwa wilaya ya Shinyanga, ambako mpaka sasa tumefikia watoto wapatao 700 na 411
tayari wamepatiwa mafunzo ya ufundi wa aina mbalimbali,”
“Kwa
upande wa mradi wa SAUTI tumefanikiwa kukusanya mabinti kutoka makundi maalumu
ambao wameunda vikundi vya uzalishaji mali na tumewapatia mafunzo ya
ujasiriamali ikiwemo ya mabadiliko ya tabia na afya, na leo hii tunakipatia
kikundi cha Wazawa Mama Lishe msaada wa shilingi milioni moja ili zikuze mtaji
wao,” alieleza.
Wageni waalikwa na Staff wa Rafiki - SDO wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro. |
Naye
meneja mradi wa Rafiki SDO, Mwamini Haruna alisema mradi wa SAUTI pia
unashughulika na utoaji wa elimu ya mabadiliko ya tabia kwa mabinti wenye umri
wa kuanzia miaka 15 hadi 24 ambapo mpaka sasa mabinti 1,560 wamepatiwa simu za
viganjani zinazoingiziwa fedha kila miezi mitatu kiasi cha shilingi 70,000.
“Kwa
upande huu mradi mpaka sasa una akiba ya vikundi kiasi cha shilingi 132,489,600
na upande wa mikopo kuna shilingi 175,991,600 ambazo walengwa wanakopeshana
wenyewe kwa wenyewe, na tayari matokeo chanya yameonekana baada ya wengi wao
kuondokana na utegemezi wa wazazi katika masuala madogo madogo,” alieleza.
Meneja Miradi wa Shirika la Rafiki - SDO, Mwamini Haruna akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa SAUTI. |
SHEREHE HIZO PIA ZILIANDAMANA NA UTOLEWAJI WA ZAWADI NA VYETI VYA KUTHAMINI KAZI KUBWA ILIYOTEKELEZWA NA WATUMISHI WA RAFIKI - SDO AMBAPO KWA UPANDE WAKE MKUU WA WILAYA ALITUNIKIWA CHETI CHA KUTHAMINI MCHANGO ANAOUTOA KWENYE ASASI ZA KIRAIA KATIKA WILAYA YAKE.
KUTUNUKU HATI:
Post a Comment