Maandamano ya wake wa polisi nchini Ufaransa. |
Zaidi ya wanawake 100 ambao ni wake wa askari polisi wakiwa na washirika wao wamefanya
maandaamno wakipinga mashambulio dhidi ya maafisa wa polisi kufuatia kuuawa kwa
afisa mmoja huko Elysee.
Wanawake hao waliokuwa na ghadhabu waliandamana
katikati ya mji siku mbili baada ya Xavier Jugele kupigwa risasi mara mbili
katika kichwa na muhalifu karim Cehurfi.
Wakati huohuo vyombo vya habari nchini Ufaransa
vinasema kuwa mtu alikuwa akijihami na kisu amekamatwa katika eneo la gare du
Nord.
Polisi hawajasema iwapo kisa hicho ni cha
kigaidi.
Katika hatua nyingine wakati nchi ya Ufaransa ikishiriki katika uchaguzi mkuu siku
ya Jumapili kwingineko maafisa wa polisi walikabiliana na
waandamanaji baada ya maandamano ya muungano wa wafanyakazi mashariki mwa
Paris, ambao walitaka kura ya awamu ya
kwanza.
Maafisa wa polisi walirushiwa vitu nao
wakalipza kuptia gesi za kutoa machozi.
Chanzo: BBC
News.
Post a Comment