TUKIO LA MADIWANI WA MANISPAA KUTOA AGIZO LA KUTIMULIWA KWA WAENDESHA BAISKELI ZA BODABODA NI MFANO MZURI WA WANANCHI KUYOKUZIELEWA SHERIA NDOGO ZA MANISPĂ€A!
NDUGU ZETU HAWA WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI ILIAGIZWA WASIBUGHUDHIWE!, KWA VILE KAZI WANAYOIFANYA NI SEHEMU YA AJIRA.
LEO BAADA YA WATU KUPATA WALOCHOKUWA WANAKIHITAJI WAMEWAONA HAWANA FAIDA TENA NA WAO NA KAZI YAO INATAJWA ETI INACHAFUA MJI WAENDE NJE YA MJI KWA LENGO LA KUPANUA MJI! AJABU HII KUPELEKA BAISKELI NJE YA MJI KUNA MAHUSIANO GANI NA UPANUZI WA MJI?
KWA NINI ISIWE KWA WENYE TAXI AU PIKIPIKI?
LAKINI TURUDI KWENYE SUALA LA SHERIA HUENDA SISI WANANCHI HATUJAELEZWA, JE, MADIWANI MLIISHA PITISHA SHERIA NDOGO "BY LAWS" YA KUPIGA MARUFUKU BIASHARA YA DALADALA KATIKATI YA MJI? KAMA JIBU NI NDIYO, JE, NI SHERIA HIYO TU NDIYO MLIYOONA IWEKEWE MKAZO KWA VILE INAWAGUSA WALALA HOI WASIOKUWA MA FEDHA ZA KUHONGA?
NAHOJI HIVI MAANA KUNA SHERIA NYINGI ZA MANISPAA ZINAVUNJWA KILA SIKU LAKINI MADIWANI WETU HAMHANGAIKI KUCHUKUA HATUA KAMA MNAVYOSHABIKIA HILI LA BAISKELI, KULIKONI?
MFANO MDOGO TU WA SHERIA ZINAZOVUNJWA HAPA MJINI, NI PAMOJA NA SHERIA INAYOZUIA MAGARI MAKUBWA KUINGIA KATIKATI YA MJI, KUWEKA VIFAA VYA UJENZI KWENYE NJIA ZA WATEMBEA KWA MIGUU INAYOVUNJWA NA MATAJIRI WENYE MADUKA YA HARDWIRE
LAKINI PIA KUNA SHERIA INAYOZUIA GEREJI BUBU MITAANI, LEO MITAA YA KAWAWA, IKELENGE NA KENYATA IMESHEHENI GEREJI ZA PIKIPIKI NA NYUMBA ZA MAKAZI KUTUMIKA KUUZA MAFUTA YA MITAMBO KINYUME CHA SHERIA, WATAALAMU NA MADIWANI WETU HAMYAONI HAYO, AKILI ZOTE ZIMEHAMIA KWA WAENDESHA BAISKELI!
SHERIA YA MIPANGO MIJI HAIRUHUSU UJENZI WA MAJENGO YA KAWAIDA KATIKATI YA MJI, LAKINI OFISI YA MKURUGENZI NDIYO INATOA VIBALI UJENZI WA NYUMBA ZA KAWAIDA KATIKATI YA MJI UNAENDELEA KAMA KAWAIDA MAANA WAHUSIKA WANATOA KIFUNGA MDOMO!
MTAA WA CONGO SASA HIVI NI KITUO KIKUU CHA MAGARI MAKUBWA YA KWENDA MINADANI, MADIWANI HAMKULIONA HILO, MMEONA BAISKELI TU! I N A S I K I T I S H A
INATIA UCHUNGU, NALAZIMIK KUAMINI KUWA SABABU KUBWA KUPIGWA MARUFUKU WENZETU WA BAISKELI INACHANGIWA NA VIONGOZI WETU WENGI NA WAKUU WA IDARA KUMILIKI PIKIPIKI, NOAH NA HAICE HIVYO BAISKELI ZINAPUNGUZA HESABU!
NIWAOMBE NENDENI KAHAMA MKAJIFUNZE WAO WALITUMIA NJIA GANI KUPUNGUZA DALADALA BARABARANI?
BAADHI YA SHERIA ZINAZONJWA NIMEKUWEKEA HAPA KWA PICHA:
Post a Comment