Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Shaaban Luseza, akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya mkutano mkubwa wa kimkoa utakaofanyika mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Nsalala kata ya Tinde wilayani Shinyanga.

JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA MKOANI SHINYANGA INATARAJIA KUFANYA MKUTANO MKUBWA WENYE LENGO LA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI WA MADHEHEBU YOTE JUU YA UMUHIMU WA KUDUMISHA HALI YA AMANI NA UTULIVU NCHINI PAMOJA NA UMUHIMU WA KUMJUA MWENYENZI MUNGU.


AKIZUNGUMZIA MAANDALIZI YA MKUTANO HUO UTAKAOFANYIKA MWISHONI MWA WIKI HII KATIKA KIJIJI CHA NSALALA KATA YA TINDE WILAYANI SHINYANGA, KIONGOZI MKUU WA JUMUIYA HIYO MKOANI SHINYANGA, SHABANI LUSEZA ALISEMA MAANDALIZI YOTE MUHIMU YAMEISHAKAMILIKA.

ALISEMA MKUTANO HUO UTAHUDHURIWA NA WATU ZAIDI YA 1,500 KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI NCHINI IKIWEMO MIKOA YA JIRANI WAKIWEMO VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA WA JUMUIYA HIYO YA AHMADIYYA NA WA KISERIKALI WAKIONGOZWA NA KAIMU MKUU WA MKOA WA SHINYANGA, JOHN MONGELLA.

AKIFAFANUA LUSEZA ALISEMA LENGO KUU LA KUFANYIKA KWA MKUTANO HUO NI KUWAKUMBUSHA WATU JUU YA UMUHIMU WA KUZINGATIA MAFUNDISHO YA MWENYEZI MUNGU AMBAYO IWAPO YATAZINGATIWA JAMII KWA UJUMLA ITAWEZA KUISHI KWA HALI YA AMANI NA UTULIVU KAMA INAVYOHIMIZWA MARA KWA MARA NA VIONGOZI WA KISERIKALI.

PIA ALISEMA KUPITIA MKUTANO HUO, JAMII ITAELIMISHWA JUU YA DHANA POTOFU DHIDI YA UISLAMU AMBAPO BAADHI YA WATU WAMEKUWA WAKIHUSISHA DINI HIYO PAMOJA NA VIKUNDI VYA KIGAIDI MFANO WA BOKO HARAAM, ISIS, AL-SHABAAB NA VINGINE VINGI.

“UKWELI UPO WAZI DINI YA KIISLAMU MISINGI YAKE MIKUU NI AMANI NA SALAMA, NA INAPINGA VIKALI SUALA LA UMWAGAJI WA DAMU YA MTU BILA SABABU, HIVYO HAWA WANAOJIITA NA KUANZISHA MAKUNDI YA UGAIDI HAPA DUNIANI HAWATOKANI NA DINI HII KWANI MWENYEZI MUNGU ANAELEZA WAZI NDANI YA KITABU CHAKE CHA KUR-AN KWAMBA, ANAYEUA MTU MMOJA NI SAWA NA KUUA WATU WOTE DUNIANI,”

“NA YULE ANAYEMNUSURU MTU MMOJA NI SAWA SAWA NA KUWANUSURU WATU WOTE DUNIANI, KWA HALI HII MAKUNDI HAYA YANAYOMWAGA DAMU ZA WATU WASIO NA HATIA HAYANA UHUSIANO WOWOTE NA DINI HII YA MWENYEZI MUNGU, NA WALA YANACHOKIFANYA HAKIWEZI KUITWA JIHADI YA KUNUSURU DINI,” ALIELEZA LUSEZA.

ALISEMA JIHADI YA KUMWAGA DAMU ZA WATU KWA KUTUMIA SILAHA MBALIMBALI IKIWEMO KUJILIPUA KWA MABOMU KWA HIVI SASA HAIPO, BALI JIHADI YA KWELI NI YA KUTUMIA KALAMU NA MANENO MAZURI KWA KUHUBIRI AMANI NA SALAMA ILI WATU WOTE ULIMWENGUNI WAWEZE KUISHI KWA AMANI.

"MTU YE YOTE ASIYEKUWA NA IMANI YA MUNGU, NI WAZI ANAWEZA KUBASHA UBAYA WOWOTE ULE KWA VILE HAKUNA ANAYEMUOGOPA, TUNAAMINI KUPITIA MADA MBALIMBALI ZITAKAOWAKILISHWA KATIKA MKUTANO WETU HUU, WATU WENGI WATAELEWA JUU YA UMUHIMU WA KUDUMISHA AMANI HAPA NCHINI, NA NI WAZI ALIYESHIBA NENO LA MUNGU SIYO RAHISI KWAKE KUTENDA VITENDO VIOVU," ALIELEZA LUSEZA.

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top