MR. HUMPHREY POLEPOLE AWACHANGANYA WATANZANIA, HANA MSIMAMO!!!!

NAHITAJI MSAADA WA HARAKA, KATIKA KIPINDI CHA MADA MOTO KINACHORUSHWA NA KITUO CHA LUNINGA CHA CHANNEL TEN, NIMEMSIKIA KWA MASIKIO YANGU, HUYU MCHAMBUZI WA MAMBO YA KISIASA KATIKA VIPINDI MBALIMBALI VYA REDIO NA LUNINGA, HUMPHREY POLEPOLE AMBAYE PIA NI MIONGONI MWA WALIOKUWA WAJUMBE WA TUME YA KUKUSANYA MAONI KUTOKA KWA WANANCHI KUHUSU MABADILIKO YA KATIBA, KATIKA MAELEZO YAKE KIDOGO AMENICHANGANYA:

1.      AMEDAI VIONGOZI WA UKAWA WAMEFANYA KOSA KUBWA KUMPOKEA MHESHIMIWA LOWASSA NA KUMPATIA NAFASI YA KUGOMBEA URAIS, HAPA NINA SWALI, HIVI KARIBUNI KUPITIA KITUO HICHO HICHO CHA LUNINGA NILIBAHATIKA KUMSIKIA, POLEPOLE HUYO HUYO, SIYO PACHA WAKE AKIWASHAURI VIONGOZI WA UKAWA WAEPUKE KUWATEUA WATU WAWILI, IBRAHIMU LIPUMBA NA DR. WILFRED SLAA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA VILE WALIWAHI KUGOMBEA NAFASI HIZO NA KUSHINDWA, HAPA ALISHAURI WATAFUTE MTU MWINGINE TOFAUTI,

2.      VIONGOZI WA UKAWA HATIMAYE WAMEWAWEKA KANDO, DKT. SLAA NA PROFESA LIPUMBA, WAMEMTEUA LOWASSA, AJABU POLEPOLE KAIBUKA TENA KWA NGUVU ZOTE AKIPINGA UTEUZI HUO KWA MADAI, LOWASSA ANA TUHUMA NYINGI NA HASTAHILI KUGOMBEA NAFASI HIYO YA JUU YA UONGOZI KATIKA TAIFA LETU.  HATA HIVYO KWA MSHANGAO MKUBWA ALISHINDWA KUJIBU SWALI LA MMOJA WA WATAZAMAJI WA KIPINDI HICHO CHA MADA MOTO, ALIYEMTAKA AMWELEZE IWAPO MGOMBEA WA CCM, JOHN MAGUFULI YEYE HANA TUHUMA ZOZOTE ZILE!!! HUYU BWANA ALICHENGA KUJIBU KWA UFASA SWALI HILO, PAMOJA NA KWAMBA KATIKA MAELEZO YAKE YA AWALI ALIKAZIA SUALA LA MGOMBEA URAIS KUTAKIWA KUWA JUU YA TUHUMA ZOZOTE ZILE!!!

3.      UKWELI NI KWAMBA VIONGOZI WENGI HAPA NCHINI WANA TUHUMA KIBAOOOOO!!!! SIJUI KWA MAONI YA MR. POLEPOLE ITABIDI WATANZANIA SASA TUMUOMBE MWENYEZI MUNGU ATUPATIE MMOJA WA MALAIKA WAKE ILI AWEZE KUWA RAIS WETU, MAANA MGOMBEA URAIS KWA MUJIBU WA POLEPOLE HAPASWI KUWA NA HARUFU YOYOTE  YA TUHUMA ZA UFISADI.

Tutafakari!!! Tuwe makini, noti zisitupeleke pabaya!!
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top