MCHEZO WA MPIRA KWA WATOTO WA KIKE. |
Mwalimu mkuu wa shule moja ya kiislamu mjini
Melbourne, Australia amedaiwa kuwazuia wasichana katika shule hiyo kutoshiriki
katika maswala ya michezo kwa hofu kwamba huenda wakapoteza ubikira.
Wanafunzi wa kike katika chuo cha Al-Taqwa
mjini Truganina pia walizuiwa kucheza soka kwa kuwa majeruhi huenda yakawafanya
kuwa tasa kulingana na fairfax.
Wasimamizi wa shule hiyo kwa sasa wanachunguza
madai hayo yaliowasilishwa dhidi ya Mwalimu mkuu Omar Hallak ambaye awali
alizua hisia kali baada ya kusema kuwa wapiganaji wa Islamic state walikuwa
wakiungwa mkono na mataifa ya magharibi.
Katika barua iliondikwa na wizara na
kuchapishwa na The Age,mwalimu mmoja wa zamani alisema kuwa:''Anaamini kwamba
iwapo wasichana wataruhusiwa kukimbia huenda wakapoteza ubikra wao.
Mwalimu huyo pia ana ushahidi wa kisayansi
unaosema kuwa iwapo wasichana watajijeruhi,kupitia kuvunjika mguu wakati
wanapocheza soka huenda ikawafanya kuwa tasa''.
Mwalimu huyo amedai kwamba Bwana Hallak
aliwazuia wanafunzi wa kike kutoshiriki katika mashindano ya wilaya ya mbio za
marathon mwaka wa 2013 na 2014.
Source: BBC
Swahili News
Post a Comment