EDWARD LOWASSA AKIKABIDHIWA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS |
JOHN MAGUFULI (CCM) AKIKABIDHIWA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS. |
Zaidi ya wiki mbili sasa vyombo vyote vya
habari vinaripoti kuhusu Lowassa. Radio, TV, Magazeti yote ni Lowassa. Either
Magufuli kaachwa mpweke au media zinampuuza.
Magazeti hayaandiki kabisa kuhusu Magufuli. Na yakiandika yanampa nafasi hafifu sana kwenye habari za kawaida. Kwa wiki mbili sasa Magufuli hatokei kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti, Na akitokea anawekwa kwenye "strap story" or "anchor story". Magufuli sio story ya kuuza gazeti tena.
Lakini Lowassa ambaye CCM wanadai ni "makapi" anaongoza vichwa vya habari kwa wiki mbili sasa. Magazeti yote ya Kiswahili na Kiingereza yanampa nafasi Lowassa kwny "Lead story". Yani Lowassa ni habari ya kuuzia gazeti. Leo magazeti 17 ya Kiswahili, magazeti 16 yameandika kuhusu Lowassa, gazeti la UHURU na HaBARI LEO tu yamempa Lead Story Magufuli.
Itz amazing kwamba Lowassa hata akikohoa tu NI HABARI, lakini Magufuli hata akisindikizwa na Rais kuchukua fomu SI HABARI. This is amazing fact ambayo mtaalamu yeyote wa media ameiona.
Siku Magufuli anachukua Fomu ya Urais pale NEC, siku hiyohiyo CHADEMA walifanya Mkutano mkuu na kumpitisha Lowassa kuwa mgombea Urais. Vyombo vyote vya habari vili-cocentrate kwenye mkutano mkuu wa CHADEMA. TV zikarusha Live, Radio zikatangaza siku nzima, magezeti yote kesho yake yakaandika kuhusu Mkutano mkuu wa CHADEMA.
Hakuna aliyejua kama Magufuli amechukua fomu hadi watu walipoona clip kwenye "whatsapp". Yani chombo cha habari kilichompa promo kidogo Magufuli ni TBC na "whstsapp". Hii ni aibu kwa Mgombea Urais kutegemea "whatsapp" kama media strategy yake. Ni wazi timu yake ya mikakati imeprove failure.
Baada ya Magufuli kuchukua fomu ya Urais Magazeti yaliyoandika kesho yake yote yalimpa Lowassa nafasi muhimu zaidi ktk gazeti "Lead Story" na habari ya Magufuli ikawekwa kama "Strap story".
Maana yake ni nini? Maana yake ni kuwa story za Magufuli hauziki? Hazina mvuto, haziandikiki. Gazeti lolote likiandika "Lead Story" ya Magufuli ni wazi siku hiyo mauzo yatashuka sana. Hakuna mtu ana muda wa kusoma habari za Magufuli labda JK na familia yake.
Lakini ukitaka gazeti lako liuze nakala nyingi sana weka habari za Lowassa. Ndio maana hata magazeti yanayomilikiwa na makada wa CCM kama MTANZANIA, MAJIRA, JAMBO LEO na JAMHURI yamempa coverage kubwa Lowassa kuliko Magufuli.
Hii ni dalili ya wazi kuwa Lowassa anauzika na kukubalika zaidi kuliko Magufuli. Pia ni wazi kuwa Timu ya Mikakati ya UKAWA ipo vizuri mara 100 zaidi kuliko timu ya Mikakati ya CCM.
Baadhi ya rafiki zangu ambao ni viongozi wa CCM wanakiri wazi kuwa tumewazidi mikakati. Nikiwa napiga nao story "off the record" wanakiri wazi kuwa "Tumewashika pabaya".
Huwezi kumwambia mgombea Urais akachukue fomu siku CHADEMA inafanya mkutano mkuu. Ni sawa na kutoa matangazo ya "dawa ya panya" siku ya ujio wa Obama. Unadhani kipi kitapewa coverage kubwa?
Source:
Jamii Forums.
Post a Comment