Kazi
ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ya kusaka wadhamini juzi nusura iingie
dosari baada ya wanachama kutaka kuchana fomu zenye orodha ya wadhamini kwa
madai kuwa hawakupewa “nauli” ya kwenda ofisi za CCM kufanya kazi hiyo.
Wakati
tafrani hiyo ikitokea mjini Mbeya, Balozi Amina Salum Ali alisema mjini Tanga
kuwa hajawahi kuona nchi ambayo mtu anaiba fedha, halafu anaambiwa azirejeshe
bila ya kuchukuliwa hatua zozote, akisema huo ni udhaifu mkubwa katika
kudhibiti ufisadi.
Katika
sakata la Mbeya, kundi la baadhi ya wanachama kutoka kata nne waliokabidhi kadi
na kuandikwa majina yao kwenye ofisi za CCM za Wilaya ya Mbeya Mjini,
liliambiwa kuwa hakukuwapo na posho kwa ajili ya kazi hiyo.
Kauli
hiyo ilisababisha wanachama hao kupora na kutaka kuchana fomu iliyokuwa na
majina yao.
Katibu
wa CCM wilaya hiyo, Kulwa Milonge alisema tukio hilo lilikuwa kubwa na
kuhatarisha usalama, lakini chama kiliingilia kati na kusawazisha mambo.
Milonge
alisema hadi mwisho wa tukio hilo, ofisa aliyetumwa na Sumaye kukusanya saini
hizo aliondoka na majina 45 ya wadhamini.
Sumaye
ni mmoja kati ya wanachama wengi waliojinadi kuwa wanachukia rushwa na ameeleza
bayana kuwa iwapo CCM itampitisha mlarushwa, atajiondoa.
Source:
Mwananchi Newspapers
Post a Comment