Askari saba wa Jeshi la Polisi nchini, kitengo
cha Usalama Barabarani, wamenusurika kifo kufuatia ajali iliyohusisha gari la
Polisi na gari moja binafsi mjini Arusha leo hii.
Ni baada ya dereva kusimamishwa akakataa, Trafiki wakapiga simu mbele, alipofika akakutwa askari wameweka kizuizi njiani akawagonga.
Taarifa ambazo bado hazijadhibitishwa na jeshi hilo zinaelewa kuwawatatu wamefariki hapo hapo.
Gari zilizohusika katika ajali hiyo, zote ni aina ya Toyota Land Cruiser, moja likiwa ni mali ya Jeshi la Polisi nchini, na jingine lenye namba T 549 ADM, ambalo ni mali ya kampuni moja ya Utalii mkoani humo.
Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa
tukio hilo, ambapo, kupitia taarifa fupi iliyopatikana kwenye mtandao wa
kijamii unaoendeshwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani, taarifa ya Jeshi hilo
imesomeka kama ifuatavyo.
Ni kweli ajali imetokea na kusababisha majeruhi
7 wakiwa ni askari wa Usalama barabarani Arusha. Chanzo cha ajali ni mwendokasi
wa dereva hatimaye kushindwa kumudu gari na kusababisha gari kuhama njia na
kugonga gari la Polisi lililokuwa linakuja mjini Arusha.
Dereva alikuwa amelewa na kwa kiwango kikubwa baada ya kupimwa. Majeruhi walipelekwa Serian hospita kwa matibabu, majeruhi wanne wameruhusiwa na watatu wamelazwa na wanaendelea vizuri.
Dereva alikuwa amelewa na kwa kiwango kikubwa baada ya kupimwa. Majeruhi walipelekwa Serian hospita kwa matibabu, majeruhi wanne wameruhusiwa na watatu wamelazwa na wanaendelea vizuri.
Source: Mitandao ya kijamii/Jamiiforums.
Post a Comment