Kumekuwa na msururu wa mashambulizi ya
maguruneti kuwalenga maafisa wa polisi katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura.
Maafisa wa usalama wanasema kuwa takriban
polisi 11 walijeruhiwa usiku kucha.
Maguruneti hayo yalirushwa katika maeneo ambayo
yaliathiriwa na maandamano ya ghasia kufuatia hatua ya rais Pierre Nkurunziza
kutaka kuwania muhula wa tatu.
Maafisa wa polisi wamewalaumu wanaharakati wa
upinzani.
Makundi ya haki za kibinaadamu yanasema
takriban watu sabini wameuawa na wengine 500 kujeruhiwa tangu maandamano hayo
yaanze mnamo mwezi Aprili.
Chanzo: BBC Swahili News
Post a Comment