Kumezuka ghasia katika mji wa Bujumbura nchini
Burundi kati ya maafisa wa polisi na waandamanaji wanaoishtumu serikali kwa
kufanya mapinduzi ya kikatiba.
Waandamanaji walirusha mawe na kuchoma matairi
huku maafisa wa polisi wakilazimika kurusha vitoa machozi na risasi bandia
hewani.
Ghasia hizo zinafuatia tangazo siku ya jumamosi
kwamba rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameteuliwa na chama chake kuwania
muhula wa tatu wa urais.
Upinzani umeitaja hatua hiyo kama ukiukaji wa
katiba,na kuonya kuwa huenda ikaathiri makubuliano ya amani ambayo yalimaliza
miaka kadhaa ya mapigano ya kikabila.
Serikali imesema kuwa maandamano hayo si
halali.
Maelfu ya raia wa Burundi wamelitoroka taifa
hilo katika majuma ya hivi karibuni wakihofia kuongezeka kwa ghasia hizo huku
taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi mnamo mwezi Juni.
Source: BBC
Swahili News
Post a Comment