Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Ngorongoro
ndugu Revocatus William Parapara (kulia) amejiondoa kwenye Chama hicho na kujiunga na
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ndugu
Parapara amefanya maamuzi hayo katika mkutano wa hadhara, eneo la Wasso,
Loliondo ambao umehutubiwa na Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye ni Katibu Mkuu wa
CCM wa Taifa ambaye anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Arusha.
Ndugu
Revocatus Parapara mekuwa Kiongozi Mwandamizi wa Chadema katika wilya ya
ngorongoro kwa Miaka zaidi ya 10. Na katika mkutano huo ndugu Parapara amesema
hawezi kuendelea kushiriki kupanda mbegu ya ubaguzi ambayo inaendelea kumea
katika Chama Chake cha zamani cha CHADEMA.
Wakati
Parapara akichomoka CHADEMA nyuma yake pia amefuatiwa na aliyekuwa Makamu
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) Bi. Elinami Limbali
amekihama Chama hicho akiongozana na Mwenyekiti wake wa Wilaya na wote
wamejiunga na CCM hali inayoonesha CCM wameanza kuramba turufu zenye mtaji
katika Jimbo la Arusha.
Wakati
wa kujiunga kwao na CCM viongozi hao waliokuwa wafuasi wazuri wa CHADEMA
walidai hatua yao hiyo inatokana na kuchoshwa na sera za kuhamasisha vurugu
badala ya maendeleo zinazofanywa na CHADEMA, na kwamba zinapotokea vurugu
watoto na akina mama ndio hupata tabu.
Post a Comment