UNICEF: Watoto Sudan K wangali wanatumiwa
vitani.
Mustakbali wa watoto nchini Sudan Kusini
umesalia mashakani hasa kwenye majimbo ya Upper Nile na Unity kutokana na
watoto kuendelea kutumiwa vitani.
Hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto
la Umoja wa Mataifa, UNICEF. UNICEF inasema watendaji wake pamoja na wadau
walioko eneo hilo wameripoti ongezeko la uandikishaji watoto jeshini mwezi
uliopita kunakofanywa na serikali na kikundi cha Johnson Olomi.
Mwakilishi wa UNICEF huko Sudan Kusini
Jonathan Veitch amesema utumikishaji watoto hawajaachiliwa huru licha ya maombi
ya kutaka pande hizo zifanye hivyo.
Amesema watoto wanaoshikiliwa wanaruhusiwa
kwenda nyumbani mchana lakini jioni ni lazima warejee kambini. Ameongeza kuwa,
"uchunguzi kuhusu masaibu ya watoto imekuwa vigumu kutokana na
vitisho dhidi ya watu na mashirika yanayojaribu kufuatilia hali ilivyo.
Amesema takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya
watoto waliotekwa huko Unity na Upper Nile mwezi uliopita inafikia mamia kwa
mwezi uliopita.
UNICEF imekumbusha serikali na upinzani Sudan
Kusini kuwa utumikishaji watoto jeshini ni ukiukwaji mkubwa wa haki zao za
msingi na kwamba warejelee makubaliano waliyosaini ya kuacha kutumikisha
watoto.
Source: Iran
Swahili Radio.
Post a Comment