KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mkazi wa Nyakato wilayani Kahama, Elias Charles (30) amekutwa amejinyonga kwa kile kilichodaiwa kukwepa deni aliloliwa akidaiwa la shilingi 150,000.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema tukio hilo lilitokea huku eneo la Nyakato wilayani Kahama ambapo mwili wa mwananchi huyo uligunduliwa na mkewe Regina William (30) wakati akitokea kuoga ukiwa unaning’inia nyuma ya mlango wa chumba chake.

Kamugisha alisema Charles alijinyonga kwa kutumia kamba aina ya manila na inahisiwa chanzo cha yeye kuchukua uamuzi huo ni kushindwa kulipa deni la shilingi 150,000 alilokuwa akidaiwa na ndugu zake.

“Tulipopata taarifa za tukio hili tulifanya uchunguzi wa awali na tumebaini chanzo cha huyo bwana kuchukua maamuzi ya kukatisha uhai wake ni deni la shilingi 150,000 analodaiwa tangu mwaka jana na siyo ugomvi kati yake na mkewe kama ilivyohisiwa awali, tunahisi aliona njia rahisi ya kukwepa deni hilo ni kujiua,” alieleza Kamugisha.

Kamugisha alisema hivi sasa mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya serikali wilayani Kahama na polisi wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top