Kamati
ya elimu katika bunge la Uingereza ilianzisha uchunguzi baada ya kubainika kuwa
zaidi ya thuluthi moja ya shule zilikuwa zikishindwa kutoa mafunzo ya somo hilo
kwa aumri unaohitajika.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo Graham Sturat amesema kuwa vijana wadogo wana haki ya kupata
habari ambazo zitahakikisha usalama wao.
Serikali
imesema kuwa itaangazia matokeo ya ripoti hiyo.
Mwaka
2013 ripoti ya bunge hilo ilisema kuwa masomo ya kibinafsi,ya kijamii ,afya na
elimu ya kiuchumi ambapo somo hilo la ngono limehusishwa yanahitaji kuimarika
katika asilimia 40 ya shule.
Wabunge
hao wamesema:Hali hii haitakubalika katika masomo mengine licha ya kuwa
harakati za serikali kuimarisha masomo hayo ni za kiwango cha chini.
Je,unakubaliana
na wazo la bunge la Uingereza kuwafunza watoto wa shule za msingi somo la ngono
na uhusiano?
Source: bbcswahili.
Post a Comment