Chama cha APPT Maendeleo, kimepinga hatua inayochukuliwa na baadhi ya
vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
kuwashawishi wananchi wasishiriki kupiga kura ya maoni kwa ajili ya
kuamua Katiba inayopendekezwa.
Katibu Mwenezi wa APPT Maendeleo Taifa, Godfrey Davis, akizungumza
na waandishi wa habari amesema kuwashawishi wananchi wasishiriki
kupiga kura, ni kosa na ni kuwanyima haki ya demokrasia ya kuamua Katiba
yao.
Davis alisema vyama vya siasa vitambue kuwa mchakato wa Katiba
umegharimu mamilioni ya fedha, hivyo ni jambo la kushangaza wakati
imefikia hatua ya mwisho kisha wanashawishi wasishiriki wakati
wanaopinga wanayo nafasi ya kupiga kura ya hapana.
Hata hivyo, alisema APPT Maendeleo inaungana na vyama vingine vya
siasa kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kusogeza mbele zoezi la
uandikishaji wapiga kura pamoja na kura ya maoni.
Alisema kimsingi muda uliobaki Nec haiwezi kukamilisha mchakato wa
kuandikisha wapiga kura wote wenye sifa na kuingia katika upigaji kura
ya maoni na kuleta ufanisi.
Post a Comment