Chanjo
kwa kawaida huifundisha kinga ya mwili wa mtu kukabiliana na maambukizi.
Lakini,watafiti
katika taasisi ya Scripps mjini Carlifornia wamebadilisha DNA ya nyani hao ili
kuzipa seli zao uwezo wa kukabiliana na virusi vya HIV.
Kikosi
hicho cha wanasayansi kimetaja hatua hiyo kama mafanikio makubwa na sasa
kinataka kuanzisha mbinu hiyo miongoni mwa binaadamu.
Majaribio
yaliofanywa miongoni mwa nyani hao katika ripoti ya jarida la asili,yalionyesha
kuwa nyani walikingwa kutokana aina yoyote ya virusi vya HIV kwa kipindi cha
wiki 34.
Watafiti
wanaamini kuwa mpango huo huenda ukawa muhimu miongoni mwa watu ambao wana
virusi vya HIV.
Mtanfiti
bingwa Professa Micheal Farza ameiambia BBC :'' tunakaribia kupata tiba ,lakini
bado tunakabiliwa na vikwazo hususan katika salama wa kuwapa watu wengi zaidi.
''Tunaifurahia
na tunadhani kwamba mi mafanikio makubwa,lakini tuna upendeleo''.
Chanjo
za HIV zimeshindwa kufanikiwa kwa kuwa virusi hivyo hujibadilisha mara kwa mara
kila vinapolengwa na dawa.
Lakini
Chanjo hii mpya hulenga eneo ambalo vurusi hivyo hujibadilisha.
Source: BBC News.
Post a Comment