Bi.
Yingluck, ambaye utawala wake uliondoshwa kufuatia mapinduzi ya jeshi mwaka
jana, tayari ametimuliwa na kupigwa marufuku kutoshiriki siasa kwa miaka
mitano.
Mwezi
mmoja baada ya kutimuliwa kwake na bunge lililoteuliwa na jeshi, sasa Yingluck
Shinawatra anakabiliwa na kesi ya uhalifu ambayo huenda akipatikana na hatia na
kahukumiwa hadi miaka kumi gerezani.
Wafuasi
wake wanalalamika kwamba ni mashtaka ya kisiasa yanayonuiwa kumharibia jina
kiongozi huyo aliyechaghuliwa kwa kura nyingi.
Wanataja
kwamba hakuna makosa yoyote ya rushwa yaliothibitishwa dhidi ya mpango huo wa
ruzuku na kueleza kwamba ni hatua yenye nia safi kuwasiaida wakulima.
Lakini
serikali ya kijeshi imetupilia mbali wasiwasi huo na kuonya kwamba Bi. Yingluck
asijaribu kutorokea katika nchi za nje kama alivyofanya kakake Thaksin miaka
sita iliyopita baada ya yeye pia kushtakiwa.
Serikali
inatafakari pia kumshtaki kwa gharama nzima ya ruzuku hiyo ambayo inasema
inagharimu dola bilioni kumi na nane.
Huku
sheria inayotumika ikiwa bado ni ya kijeshi,huenda pasiwepo maandamano yoyote
ya kupinga namna anavyotendewa Yingluck.
Lakini
masaibu yake yanasukuma zaidi ahadi ya jeshi kuidhinisha upatanishi liliyotoa
wakati lilipoipindua serikali mwaka jana.
Chanzo cha habari: Swahili BBC News.
Post a Comment