UNAIKUMBUKA HADITHI HII YA KWELI YA:-
Msichana
mhindi Sarika Patel kutoka familia tajiri na Timothy Khamala mbukusu
kutoka familia maskini kutoka Magharibi mwa Kenya kuoana? wakati yao
mapenzi yao yalijulikana kama
Bukusu Darling, sifa kwa wanakoishi wawili hao.
Taarifa sasa
ni kwamba mapenzi yao yamefika kikomo. Familia ya msichana Sarika
ililaani sana mapenzi hayo kwani Timothy alikuwa anafanya kazi kwao kama
mfanyakazi wa nyumbani.
Na Sarika alipoamua kwenda kuishi na Timothy kama mume na mke familia yake ilimfukuza na kisha kumfuta kazi Timothy.
Wawili
hao walioana kinyume na matakwa ya familia ya Sarika ambayo kwao
ilikuwa ni kama aibu kubwa sana kwa mtoto wao kutoka familia tajiri
kuolea na kijana asiyekuwa na mbele wala nyuma.
Wakati taarifa ya
wawili hao ilipogonga vichwa vya habari nchini Kenya, Sarika na mume
wake walipata kazi katika kiwanda cha kutengeza Sukari kutoka kwa
wahisani.
Lakini sasa kuna madai kwamba ndoa yao imevunjika baada
ya Sarika kulalamika kwamba Timothy amekuwa akimdhulumu na kumtusi kila
mara hali iliyosababisha wawili hao kutalakiana.
Mtandao wa
Standard Digital umemnukuu Sarika akisema: "nilipokuwa mgonjwa , hakuwa
hata na muda wa kunipeleka hospitalini badala yake wazazi wake ndio
walionipeleka kutafuta matibabu. Mbali na hayo amekuwa akinichapa, ''
alisema Sarika huku akibubujikwa na machozi.
Kwa sasa inaarifiwa anajuta sana kwa nini alikaidi amri ya wazazi wake.
''Ninajuta
sana kwa nini sikuwasikiliza wazazi wangu na kuolewa kinyume na mapenzi
yao. Ninaomba radhi, natumai watanikubali kurejea nyumbani. ''
Sarika
ambaye ni mtoto wa nne katika familia ya watoto watano, ameamua kurejea
nyumbani na kusema kamwe hatawahi kuwa na uhusiano wa kimepenzi tena.
Lakini wazazi wake wamempa masharti, mwanzo aishi na rafiki yake huku
akifanya uamuzi wa mwisho kuhusu anakotaka kuishi.
Anasema
anahofia kwamba jamii ya wahindi haitamkubali tena kwani hakuwasikiliza
wakati walipomshauri kutoolewa na mwanamume mwafrika.
Post a Comment