Hayat Sheikh Abdulah enzi za uhai wake. |
Maelfu ya viongozi na wananchi wa nchi ya Saudi Arabia wakiwa wamebeba mwili wa Hayati Sheikh Abdulah tayari kwa ajili ya mazishi yake. |
Mazishi ya mfalme wa Saudi Arabia Abdulla
ambaye amega dunia yamefanyika nchini Saudi Arabia.
Mwili wake ulipelekwa msikitini kuswaliwa
katika mji mkuu wa nchi hiyo Riyadh kabla ya kuzikwa.
Viongozi kadhaa wa nchi za kiarabu na marafiki
za Asudi Arabia walihudhuria mazishi hayo.
Awali mfamle mpya nchini Saudi Arabia Salman
bin Abdul-Aziz al Saud alisema kuwa ataendeleza sera za mtangulizi wake ambaye
aliaga dunia jana alhamis baada ya kuugua ugonwa wa nimonia.
Katika hotuba iliyotolewa kupitia kituo cha
runinga cha taifa mfalme huyo pia alitoa wito wa kutaka kuwepo amani miongoni
wa nchi za kiarabu.
Wizara muhimu zikiwemo ya mambo ya kigeni,
mafuta na fedha hazijafanyiwa mabadliko.
Wizara wa ulinzi ambayo awali ilikuwa
inasimamiwa na mfalme mpya itaongozwa na mwanawe wa kiume Mohammed bin Salman.
Viongozi wengi wa dunia wametuma risala za
rambi rambi kwa utawala wa Saudia kufuatia kifo cha mfalme wao Abdullah.
Nchi kama vile Bahrain na Jordan zimetangaza
siku arobaini za maombolezi kwa heshima yake.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon,
amempongeza mflame huyo kwa juhudi zake za kutafuta amani katika mashariki ya
kati.
Japo mfalme Abdullah amesifiwa ndani ya nchi
yake na hata baadhi nje ya nchi, wanaharakati wa haki za binadamu wamejitokeza
kukashifu utawala wake wakisema kuwa alileta mabadiliko machache sana ya
kusifika.
Saudi Arabia ina ushawishi mkubwa katika
mataifa ya Pakistan, Bangladesh na India ambapo inafadhili miradi kadha na
shule nyingi zinazotoa mafunzo ya kidini.
Makundi nchini pakistan kwa muda mrefu yamekuwa
yakishutumu baadhi ya shule hizo ambazo yanasema zinaendesha kampeni za chuki
dhidi ya Washia.
Chamgamoto inayomkabili mfalme huyo mpya ni
kuhakikisha kuwa msaada wa mamilioni ya ya dola hauwafikii wale wanaounga mkono
chuki.
Makundi ya haki za binadamu yanaamini kuwa
uongozi mpya wa saudi Arabia utatekeleza ahadi za muda mrefu za kuboresha
mazingira kwa mamilioni ya wafanyikazi wahamiaji kutoka nchi za Asia.
Post a Comment