HILI NDILO KOMBE LA FA.

Mchezaji wa Chelsea akiwa amebanwa vilivyo na wachezaji wawili wa timu ya Bradford City.
Manchester City, Chelsea Southampton na Totenham zimeondolewa katika mechi za kombe la FA baada ya kuadhibiwa na timu kutoka daraja la chini la ligi ya EPL.
 
Timu hizo ambazo zinaongoza katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza zilishangazwa baada ya kushindwa nyumbani na wapinzani wao.

Hii ni mara ya pili kwa mabingwa wa ligi ya Uingereza Mancity kuondolewa nyumbani na Middlesborough ambao walishinda kwa 2-0.

Vilevile kilabu ya daraja la kwanza Bradford City ilionyesha mchezo wa hali ya juu ilipotoka nyuma 2-0 na kuweza kuwashinda viongozi wa ligi ya Uingereza Chelsea  kwa magoli 4-2 katika mechi ya FA iliyojaa mbwembwe za aina aina.

Katika uwanja wa Totenham bao la Jeffrey Schlupp lilisaidia Leicester kuishinda Totenham.

Leicester ilikuwa nyuma kwa bao moja kabla ya kusawazisha na kuongeza la ushindi.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top