Mwenyekiti
wa BAWACHA Taifa, Halima Mdee akipokea kadi ya CCM kutoka kwa aliyekuwa
Katibu Mwenezi wa CCM, Tawi la Jikolile kata ya Ndembezi Manispaa ya
Shinyanga, Robert Ng'welo baada ya kada huyo kuamua kujiunga na CHADEMA
juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Shinyanga. Kulia
aliyekaa chini mwenye miwani ni kada mwingine wa CCM, Joseph Rweyemamu
ambaye pia alijiunga na CHADEMA on


MWENYEKITI wa Taifa wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA),
Halima Mdee amewataka wakazi wa Shinyanga waache kulalamika na kupiga
kelele wakituhumu kuibiwa kura za ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita
mwaka 2010 ambapo alitoa wito wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na
kwenye upigaji kura.



Mdee alitoa wito huo katika mkutano wa
hadhara uliofanyika mjini Shinyanga kwenye viwanja vya Mahakama ya
Mwanzo ikiwa ni moja ya harakati za chama chake kuwaelimisha wananchi
juu ya umuhimu wa kuikataa katiba pendekezwa iliyopitishwa hivi karibuni
kutokana na kutupilia mbali sehemu kubwa na maoni yaliyotolewa na
wananchi.



Huku akishangiliwa Mdee alisema anashangazwa na kauli
za wananchi wa Shinyanga kudai katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010
waliibiwa kura za ubunge jimbo la Shinyanga mjini na kwamba aliyekuwa
ameshinda katika uchaguzi huo ni mgombea wa CHADEMA, hayati Philipo
Shelembi na ushindi wa mbunge wa CCM aliyepo ulitokana na kura
kuchakachuliwa.



Alisema hata kama ushindi wao ulichakachuliwa
hiyo ilisababishwa na uzembe na woga wao wa kutokubali kulinda kura zao
na wengine wakishindwa kwenda vituoni kupiga kura kutokana na
kutokujiandikisha kwa wingi na kwamba ili kuishinda CCM inahitajika
nguvu kubwa kama walivyofanya wapiga kura wa jimbo lake la Kawe jijini
Dar es Salaam.



“Ndugu zangu wana wa Shinyanga, acheni kukaa
mkilalamika kwamba 2010 mliibiwa kura zenu, ni ninyi wenyewe hamkukaza
buti sawasawa, kama mngekuwa imara hakuna kura hata moja ambayo
ingepotea, kama ni suala la CCM kuiba kura, basi wangekuwa na uwezo huo
katika jimbo langu ambako serikali yote ndiyo makazi yake kuanzia Ikulu
ya Magogoni hadi usalama wa Taifa,”



“Vijana wa Kawe walisimama
kidete wakakaza buti zao, hakuna ujanja wowote uliofanyika, leo hii
ninapoongea Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa watu wa Jimbo langu,
mawaziri na viongozi wakuu mbalimbali wa serikali mimi ndiyo mbunge wao,
tulikaza buti kwelikweli bila kulegeza, kuing’oa CCM madarakani
kunahitaji juhudi si mchezo,” alieleza Mdee.



Kutokana na hali
hiyo aliwaomba vijana na wanachama wote wa CHADEMA kujitokeza kwa wingi
katika kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi
wa serikali za mitaa na daftari la kudumu mwakani na kwamba kila mmoja
wao ahakikishe anakwenda kupiga kura bila kukosa na wazilinde kura zao
ili zisiibwe.



Katika hatua nyingine Chama cha Mapinduzi (CCM)
katika mkutano huo kilipata pigo baada ya kuwapoteza makada wake wawili
waliojiunga na CHADEMA  wakidai kuvutiwa na hotuba iliyotolewa na
mwenyekiti huyo wa BAWACHA Taifa aliyesema lengo la CHADEMA ni
kuhakikisha nchi inapata ukombozi wa pili utakaowawezesha watanzania
kufaidi raslimali zilizopo nchini.



Hali hiyo ilijitokeza baada ya
makada hao kukatisha hotuba ya Mdee walipoingia katikati ya uwanja
wakiinua mikono juu kwa madai wanataka kuokoka hali iliyowashangaza
wananchi katika mkutano huo huku wakifuatwa na Red Bridged waliowafuata
kwa lengo la kutaka kuwatoa hata hivyo waliposema wanataka kujiunga na
CHADEMA walishangiliwa kwa nguvu na wananchi.



Makada walioamua
kuhama CCM na kujiunga na CHADEMA ni pamoja na aliyekuwa katibu mwenezi
wa CCM Tawi la Jikolile kata ya Ndembezi, Robert Ng’welo na Joseph
Rweyemamu aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kolandoto ambao
wote kwa pamoja na walimkabidhi Mdee kadi zao za CCM na kupewa za
CHADEMA.



Kwa upande wake Mdee aliwapongeza makada hao kwa kuuona
ukweli na kuwataka wana CCM wengine wenye nia nzuri na Taifa leo
kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA ili waunganishe nguvu
kupitia Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) kuing’oa CCM madarakani
ambayo daima imeshindwa kuwaletea maisha mazuri.

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top