Mwenyekiti wa TANADA Taifa, Marco Mahecha akitoa maelezo mbele ya wajumbe wa mkutano wa mawakala wa pembejeo. |
Mahecha akifafanua baadhi ya mambo ndani ya mkutano. |
Hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kukomesha vitendo vya udanganyifu vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya mawakala wasio waaminifu huku wengine wakidiriki kusambaza pembejeo zisizo na ubora ikiwemo mbegu na viuatilifu hali iliyosababisha malalamiko mengi kutoka kwa wakulima.
Akitangaza rasmi mabadiliko hayo katika mkutano wa mawakala wa pembejeo za kilimo kutoka kanda ya ziwa uliofanyika mjini Shinyanga, Mkurugenzi msaidizi kitengo cha pembejeo kutoka wizara ya kilimo, chakula na ushirika, Canuth Komba alisema kuanzia msimu wa mwaka 2014/2015 pembejeo zote zitasambazwa kwa mfumo mpya.
Akifafanua kuhusu mfumo huo mpya, Komba alisema hivi sasa wakulima watawajibika kujiundia vikundi katika maeneo yao ambavyo vitatambulika kisheria ambavyo vitafungua akaunti benki na kutakiwa kulipia asilimia 20 kama malipo ya awali ya kiasi cha pembejeo watakazokuwa wanahitaji kununua kwa msimu husika.
“Chini ya mfumo huu mpya, vikundi sasa ndivyo vitakavyowajibika kufunga mikataba na makampuni ya usambazaji wa pembejeo za kilimo na pia vitaweka dhamana ya wakulima ili kuweza kukopeshwa pembejezo hizo,”
“Makampuni ya uzalishaji na usambazaji wa pembejeo yatapaswa kusambaza pembejeo zenye ubora kwa wakati na kutoa taarifa za mawakala wake kwa kila wilaya, kuingia makubaliano maalum na mabenki na wakulima na kupeleka bei elekezi ya pembejeo katika wilaya husika kabla ya msimu kuanza,” alieleza Komba.
Kwa wa halmashauri za wilaya zitatakiwa kuainisha idadi ya vikundi vya wakulima vyenye sifa ya kukopesheka, kuhakiki mahitaji ya pembejeo kwa kila kikundi na kusaidia kutafuta masoko ya mazao ya wakulima sambamba na kuimarisha huduma za ugani.
“Serikali hivi sasa itaweka fedha katika mabenki bila ya kutoza riba ambapo itakuwa na aina mbili za mifuko kuzalisha riba, mfuko wa dhamana na mfuko wa kupunguza riba, benki za biashara zitakopesha kwa uwiano wa 1:2, iwapo serikali itaweka shilingi bilioni 100 kwenye mfuko, mabenki yatawakopesha wakulima jumla ya shilingi bilioni 200,”
“Mfuko wa dhamana utatumika kulipia mikopo endapo yatatokea mafuriko, kiangazi au milipuko ya magonjwa au mazao kushambuliwa na wadudu waharibifu mfano wa nzige na kweleakwelea hii ni tofauti na mfumo wa awali ambapo ilipotokea matatizo mkulima bado aliwajibika kulipia pembejeo alizopewa,” alieleza Komba.
Komba alisema hivi sasa wizara ya kilimo ina jukumu la kuhakikisha inatenga fedha na kuziweka katika taasisi za fedha, kuandaa makubaliano maalum na taasisi za fedha jinsi ya kukopesha fedha za pembejeo kwa wakulima, kuelimisha wadau wa kilimo kuhusu mfumo mpya na kuratibu na kuusimamia ili pembejeo ziwafikie wakulima.
Post a Comment