Diwani wa kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga akisukumwa baada ya kupokea vibao kutoka kwa mmoja wa vijana wa UVCCM alipovamiwa na vijana hao waliokwa eneo la viwanja vya ofisi za CCM Shinyanga mjini wakiwa wamezifunga ofisi hizo wakishinikiza kuondolewa kwa katibu wa CCM wilaya, mwenezi na mchumi katika wilaya hiyo.
Hapa anajihami baada ya kupokea makofi matatu kutoka kwa UVCCM aliyeko mkono wa kulia.
Msamaria mwema akijaribu kuzuia vijana wa UVCCM wasiendelee kumsulubu diwani wa CHADEMA.
Hapa anamuondoa eneo la tukio.
Baadhi ya vijana wa CCM waliokuwa wameifunga ofisi ya CCM wilaya ya Shinyanga mjini kwa masaa kadhaa.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Shinyanga mjini wamemshambulia kwa kipigo diwani wa kata ya Ndala manispaa ya Shinyanga, Sungura George waliyemvamia alipokuwa akipita jirani na ofisi za Chama hicho.
Vijana hao wa CCM walikuwa wametanda katika ofisi hizo za CCM wilaya huku wakiwa wamefunga mlango mkuu wa kuingilia katika ofisi kwa kutumia jukwaa kubwa kwa lengo la kumzuia katibu wa CCM wilaya, Charles Sangula asiingie ofisini.

Pia vijana hao wanashinikiza kuondolewa madarakani kwa katibu mwenezi wa wilaya, Charles Shigino na yule wa mipango na fedha, Ahmed Mapalala wakiwatuhumu kuwasaidia wagombea wa CHADEMA kuibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni ambapo CCM iliambulia mitaa 26, huku CHADEMA ikibeba viti 30.
 
Aidha wamemuomba mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete na katibu mkuu, Abdulrahman Kinana wachukue hatua mara moja za kuwaondoa madarakani watendaji hao wanaohisiwa kuwa na mikakati michafu ya kutaka kukiuza chama hicho na kwamba kitendo chao kinaweza kuleta madhara makubwa katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.
 
Diwani Sungura George alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuvamiwa na vijana hao alipokuwa akitokea katika  ofisi za idara ya afya manispaa ya Shinyanga walipoamua kushambuliwa kwa kuchapwa makofi matatu na kutakiwa kupotea katika eneo hilo mara moja huku akinusurika kugongwa na gari.  
 
George alisema kufuatia shambulio hilo tayari amefungua mashitaka polisi ili vijana waliomshambulia waweze kufikishwa mahakamani.
 
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top