Na Suleiman Abeid,
Shinyanga
CHAMA Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimetamba kwa kudai huenda kikaibuka na ushindi mkubwa katika majimbo ya ubunge mkoani Shinyanga katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.viti vya ubunge.
Hali inatokana na wagombea ambao chama hicho kimewasimamisha katika majimbo yote ya mkoa wa Shinyanga kuwa ni wale wanaokubalika na wapiga kura na kwamba iwapo uchaguzi utakuwa huru na haki ni wazi wataibuka na ushindi mkubwa katika majimbo mengi.
Akizungumza na Majira Jumapili jana, mwenyekiti wa mkoa wa CHADEMA, Bw. Philipo Shelembi alisema chama chake kimejitahidi kutafuta wagombea ambao kinaamini ni wazuri na wanakubalika kwa wapiga kura.
“Safari hii hawa jamaa zetu wa CCM wafunge nguo zikaze, kwa kweli tumepata wagombea wazuri na waokubalika, wengine wao wenyewe CCM wamewafanyia faulo za makusudi, wakawaangusha, sasa tumewadaka sisi, hawa si ‘makombo’ ni lulu kwa wananchi tunaamini wanakubalika,” alieleza Bw. Shelembi.
Hatua ya chama hicho kutamba inafuatia kuwapata makada wawili maarufu wa CCM ambao walienguliwa katika kura maoni na wakaamua kujiengua na kujiunga na CCM akiwemo Bw. John Magale Shibuda anayegombea jimbo la Maswa magharibi.
Wagombea wengine katika jimbo hilo ni Bw. Robert Kisena (CCM), Bw. Seif Baya (CUF), Bw. Silas Kilolelo (TLP), Bi. Lyidia Mawala (UDP) na Bw. Mathias Jibina (NLD).
Katika jimbo la Bukombe CHADEMA kimempata Profesa Kulikoyela Kahigi, ambapo CCM wamemsimamisha mbunge wa zamani, Bw. Emmanuel Luhahula.
Jimbo la Kisesa, Bw. Erasto Tumbo (CHADEMA), Bw. Luhaga Mpina (CCM), Meatu, Bw. Salumu Khamis (CCM) na Bw. Opulukwa Jeremiah (CHADEMA).
Jimbo la Shinyanga mjini, Bw. Philipo Shelembi (CHADEMA), Bw. Steven Masele (CCM) na Bw. Maalim Mohamed Mbukuzi (CUF), Jimbo la Solwa, Bw. Julius Kasenga (CHADEMA), Bw. Ahmed Ally (CCM) na Bw. Shashu Lugeye (CUF).
Bariadi Magharibi, Bw. Zacharia Makono (CHADEMA), Bw. Andrew Chenge (CCM) na Bw. Isaack Manjolo Cheyo (UDP), Bariadi Mashariki, Bw. John Cheyo (UDP), Bw. Martine Makondo (CCM) na Bw. Matondo Makula (CUF).
Kwa upande wa jimbo la Maswa Mashariki CHADEMA kimempata Bw. Sylivestar Kasulumbayi, Bw. Peter Bunyongoli (CCM), Bi. Hamisa Philipo (CUF), Bi. Elizabeth Masunga (NLD) na Bw. Robert Masungu (UDP).
Jimbo la Kishapu Bw. Maghembe Kanoga (CHADEMA), Bw. Suleiman Nchambi (CCM) na Bw. Kizito Kashinje (UDP)
Seif Baaya (CUF), Silas Kilolelo (TLP), Lyidia Mawala (UDP) na Mathias Jibina (NLD).
Maswa Mashariki ni Peter Bunyongoli (CCM), Anifa Philipo (CUF), Robart Masunga (UDP), Elizabeth Masangu (NLD), na Silvester Kasulumbayi (CHADEMA).
HATIMAYE Bw. John Magale Shibuda amerejesha rasmi fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la Maswa Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kujiengua kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Bw. Shibuda aliamua kukihama Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kushindwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho ambapo aliangushwa na Bw. Robert Kisena ambaye ndiye aliyeteuliwa kukiwakilisha chama hicho katika nafasi ya ubunge kwa jimbo la Maswa Magharibi.
Mwana CCM mwingine aliyejiengua ndani ya Chama hicho baada ya kushindwa katika kura za maoni ni Profesa Kulikoyela Kahigi aliyekuwa akigombea katika jimbo la Bukombe ambaye pia amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Profesa Kahigi pia amechukua fomu kwa ajili ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA katika jimbo la Bukombe baada ya kuangushwa katika kura za maoni na mbunge wa zamani Bw. Emmanuel Luhahula.
Hatua ya Profesa Kahigi kuamua kugombea kupitia CHADEMA imepokelewa kwa shangwe kubwa na wakazi wa Bukombe ambapo jana hiyo mara baada ya kurejesha fomu zake umati wakazi hao waliingia mitaani wakiandamana na kushangilia kwa shangwe wakidai kuwa Profesa ndiyo mbunge wao.
Katika Jimbo la Bariadi Magharibi waliochukua fomu na kurejesha hiyo jana ni pamoja na mbunge wa zamani, Bw. Andrew Chenge (CCM), Bw. Isaack Manjolo Cheyo (UDP) na Bw. Zacharia Makono (CHADEMA).
Waliojitokeza jimbo la Bariadi Mashariki ni, Bw. John Cheyo (UDP), Bw. Matondo Makula (CUF) na Bw. Martine Makondo (CCM), kwa upande wa Meatu ni, Bw. Salumu Khamis Salumu (CCM) na Bw. Opulukwa Meshack Jeremiah (CHADEMA).
Jimbo la Kisesa, Bw. Luhaga Joelson Mpina (CCM) na Bw. Erasto Tumbo (CHADEMA) ambapo kwa jimbo la Solwa ni, Bw. Shashu Lugeye (CUF), Bw. Ahmed Ally Salum (CCM) na Bw. Julius Kasenga (CHADEMA).
Kwa upande wa Shinyanga mjini, Bw. Steven Masele (CCM), Bw. Philipo Shelembi (CHADEMA) na Mwalimu Mohamed Mbukuzi (CUF), Kahama, Bw. James Lembeli (CCM), Bw. Hamisi Makapa (CUF), Bw. Charles Lubala (CHADEMA) na Bw. Ibeshi Kaji (UDP).
Jimbo la Mbogwe, Bw. Augustine Masele (CCM), Meja Mstaafu Cleoface Magere (CUF) na Bi. Frola Msabila (CHADEMA), Kishapu, Bw. Suleiman Nchambi (CCM) Bw. Kizito Mayala (UDP) Bw. Paul Kanogu (CHADEMA), Jimbo la Msalala Bw. Ezekiel Maige (CCM), Bw. Edward Mlolwa (CHADEMA) na Bw. Dauda Hassan (CUF).
Kwa upande wa Jimbo la Maswa Mashariki Bw. Peter Bunyongoli, (CCM) na aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa CHAUSTA Tanzania bara Bw. Sylvester Kasulumbai ambaye amekihama chama hicho na kujiunga na (CHADEMA).
Mwisho.
MAKALA:
WALINZI WA JADI ‘SUNGUSUNGU’ SHINYANGA KUJIKITA KATIKA MAENDELEO: -
· Waamua kujenga shule ya sekondari ya Kisasa.
Na Suleiman Abeid,
JESHI la Jadi au walinzi wa Jadi maarufu kama ‘sungusungu’ au ‘wasalama’ si neno geni miongoni mwa watanzania wengi hivi sasa hususani kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa ya Mwanza na Shinyanga, ni moja ya vikundi vya kijamii vinavyojishughulisha na ulinzi katika maeneo yao.
Mara nyingi jeshi hili ama walinzi hawa wa jadi wamekuwa wakionekana kama vile uwepo wao si wa kisheria na hivyo kuwepo na mgongano kati yao na jeshi la polisi hasa pale inapotokea sungusungu kuhusishwa na tukio la mauaji linalosababishwa na wananchi wenye hasira kali.
Hata hivyo pamoja na matatizo ya hapa na pale yaliyokuwa yakijitokeza kuhusiana na suala la walinzi wa jadi, ikiwemo tatizo la kudaiwa kutumia nguvu kubwa wanapowaadhibu watuhumiwa wanaowakamata, lakini ukweli unabaki palepale kuwa wamesaidia sana katika suala zima la ulinzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo kudhibiti wizi wa mifugo.
Chimbuko la ulinzi huu wa jadi linatokana na wanachi wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambao mwishoni mwa miaka ya sabini waliamua kuanzisha ulinzi huo baada ya kukithiri kwa vitendo vya wizi wa mifugo katika maeneo yao.
Hali hiyo ndiyo iliyosababisha kuuanzishwa kwa ulinzi huo ambapo kwa wakati huo walitumia jina la ‘Wasalama,’ ulinzi ambao kwa sehemu kubwa ulisaidia kupunguza tatizo hilo la wizi wa mifugo katika maeneo yao.
Walinzi hawa waliendelea kupata sifa kutokana na jinsi walivyoweza kukabiliana na wezi wa mifugo katika wilaya hiyo ya Kahama ambapo polepole walianza kuenea katika wilaya jirani za mkoa wa Tabora na pia wilaya nyingine za mkoa wa Shinyanga.
Kutokana na kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na walinzi hawa wa jadi hatimaye serikali mwanzoni mwa miaka ya themanini ilianza kuwatambua rasmi chini ya aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, Bw. Augustine Lyatonga Mrema, ambapo ilihimizwa suala la ulinzi huo kuenea katika maeneo mengine nchini.
Kutambuliwa kwa walinzi hawa wa jadi kulitokana na uhaba wa askari wa Jeshi la Polisi nchini, hivyo ilikubalika kuwa iwapo jeshi hili la jadi litaweza kusaidiana na polisi wachache waliopo, suala la kulinda na kudumisha amani na usalama wa wananchi na mali zao litaimarika zaidi.
Pamoja na kwamba baadhi ya wananchi wengi hasa wale wa maeneo ya mijini wanaupinga ulinzi wa sungusungu, lakini ukweli ni kwamba ulinzi huu upo kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kwa mujibu wa kifungu namba 11 cha Sheria ya mwenendo wa Mashtaka Na. 9/1985 Sura ya 20 Revised Edition 2002, askari polisi, mwanamgambo au sungusungu wanaruhusiwa kumkamata mhalifu ye yote yule, hata hivyo kifungu cha 12 cha sheria hiyo kinazuia askari polisi, mgambo au sungusungu kumpiga au kumjeruhi mtuhumiwa.
Pamoja na kuwepo na sheria hiyo lakini walinzi hawa wa jadi nao walijiwekea kanuni na taratibu zao katika uendeshaji wa shughuli zao za ulinzi.
Moja ya kanuni yao kuu ni kuapishana, maarufu kama ‘Kutemya.’ Utaratibu huu hufanyika kwa lengo la watu wanaoamua kujiunga rasmi na ulinzi wa jadi kula kiapo na kuelezwa taratibu zote za ulinzi huo.
Moja ya kanuni za walinzi hawa wa jadi katika mikoa hii ya Mwanza na Shinyanga juu ya mtuhumiwa anayekamatwa kwa makosa mbalimbali kijijini ni kumlipisha faini maarufu kwa jina la ‘mchenya.’
Hii hufanyika baada ya mtuhumiwa wa kosa lolote kukamatwa ambapo huwekwa katika baraza la sungusungu la kijiji na baada ya kuelezwa makosa yake hutakiwa alipe ‘mchenya’ huo ambao mara nyingi huwa ni ng’ombe kadhaa au kiasi cha fedha kulingana na hali ya kimapato ya mtuhumiwa.
Mtuhumiwa aliyepatikana na hatia na kupewa adhabu hiyo ya kulipa faini ‘mchenya’ wa ng’ombe au fedha hutengwa na jamii mpaka pale atakapokuwa ametekeleza adhabu yake, mtuhumiwa anayetengwa haruhusiwi kuingia katika nyumba ya mkazi ye yote kijijini au kuongea na mtu ye yote na hata kama atakwenda katika kisima cha maji, basi jamii humpisha kwanza achote maji na aondoke ndipo wengine waendelee.
Chini ya utaratibu huu wa kukusanya ‘mchenya’, walinzi hawa mara nyingi mapato waliyokuwa wakiyapata yalikuwa hayatumiki kwa shughuli yoyote ya maendeleo ambapo utaratibu waliokuwa wamejiwekea hupanga siku maalumu kama sherehe ambapo ng’ombe wote waliotolewa kama ‘mchenya’ huchinjwa na watu kula nyama na vinywaji vinavyonunuliwa kutokana na fedha ya mchenya.
Utaratibu huu umedumu kwa muda mrefu sasa, pamoja na juhudi za viongozi wa serikali kuwataka viongozi wa sungusungu kuachana na utaratibu huo lakini ilikuwa ni vigumu kutokana na mazoea ya walinzi wenyewe hasa pale inapozingatiwa kuwa mali hiyo ni ya wengi hivyo kutumiwa na wenyewe kwa kula nyama ilikuwa ndiyo njia muafaka.
Hata hivyo juhudi za viongozi wa serikali hasa kwa mkoa wa Shinyanga hivi sasa zimeonesha kuzaa matunda ambapo viongozi wa sungusungu wa mkoa kwa kauli moja wameamua kubadilika na kukukubaliana kutumia mapato wanayokusanya kutoka katika michenya kwa kufanya shughuli za maendeleo.
Wakizungumza katika kikao maalumu na mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Dkt. Yohana Balele, wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za Nane nane zilizofanyika kimkoa katika wilaya ya Meatu, viongozi hawa wamesema hivi sasa wameamua kujenga shule moja ya sekondari ambayo itakuwa ni kumbukumbu ya shughuli zao.
Katibu wa sungusungu hao Bw. John Kadama anasema, “…sisi walinzi wa jadi, baada ya kukaa na kutafakari kwa makini tumeona kuwa suala la kukusanya michenya na kuitumia kwa kula nyama hivi sasa limepitwa na wakati,”
“Kutokana na hali hiyo tumeamua kubadilika, tumeona ni vizuri tukatumia mapato tunayokusanya kutoka kwa watuhumiwa tunaowapiga ‘michenya’ tuyatumie kwa shughuli za maendeleo, na kwa kuanzia tumeamua kujenga shule moja ya sekondari ya sungusungu katika eneo la Mwalugoye katika Manispaa ya Shinyaga,”
“Tunaamini shule hii itakapokamilika itakuwa ni kumbukumbu muhimu ya shughuli zetu kwa vizazi vijavyo, na tumefikia uamuzi huu baada ya kubaini kuwa mkoa wetu bado uko nyuma sana katika suala zima la elimu, sasa badala ya kukaa na kula nyama tumeamua kujenga shule, ambayo inakisiwa itatugharimu zaidi ya shilingi milioni 400.”
Bw. Kadama anasema shule hiyo itakapokamilika itasaidia kuongeza idadi ya shule za sekondari mkoani Shinyanga, na kwamba sekondari hiyo itaanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita, na kwamba tayari hivi sasa wameshalipia kiwanja na hatua inayofuata itakuwa ni kuandaa michoro ya shule hiyo.
“Baada ya kupata gharama zote za ujenzi wa sekondari tunayokusudia kuijenga, uongozi wa sungusungu ngazi ya mkoa katika kikao chake kilichofanyika hivi karibuni umekubaliana kugawana gharama hizo kwa kila wilaya, ambapo sungusungu wote watachangia, gharama halisi tulizopigiwa ni shilingi 435,783,710,” anaeleza Bw. Kadama.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga ameupongeza uamuzi huo wa sungusungu kwa kuweza kuona tatizo kubwa linaloukabili mkoa wao, ambalo ni ukosefu wa elimu kwa wakazi wake.
“Ninakupongezeni sana kwa uamuzi huu wa busara, kwa kweli suala la kukaa na kula nyama kila mara lilikuwa siyo zuri, mkoa wetu una matatizo mengi, hasa ujinga miongoni mwa wakazi wake, kwa hatua hii mliyoamua mnastahili pongezi,”
“Hata hivyo ni vizuri sasa Halmashauri zetu za wilaya zikashirikiana nanyi katika ujenzi huu mlioamua kuuanzisha, na pia wachangie ujenzi wa sekondari hiyo, shule hii haitasomesha watoto wa sungusungu pekee bali jamii nzima itanufaika, ni vizuri ukawepo ushirikiano wa karibu ili yawepo mafanikio,” anaeleza Dkt. Balele.
Hata hivyo mbali ya uamuzi huo wa ujenzi wa sekondari ya kiasasa ya sungusungu, Dkt. Balele amewataka walinzi hao wa jadi hivi sasa kuhakikisha wanasaidia katika kukomesha mauaji ya vikongwe ambayo yanatia aibu na kuvunja haki za binadamu.
Anasema, “Mmekuwa mkifanya juhudi kubwa katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika maeneo mengi mkoani petu, hasa kuwasaka na kuwakamata wezi wa mifugo, lakini ajabu hamjaweza kusaidia kumaliza tatizo la mauaji ya vikongwe, tatizo ambalo limekuwa sugu katika mkoa wetu,”
“Sasa kuanzia leo nakuombeni na ninawaagiza sungusungu wote kuhakikisha wanawasaka na kuwafikisha katika vyombo vya dola watuhumiwa wote wa mauaji ya vikongwe, nafikiri uwezo huo mnao, iweje wezi wa ng’ombe mnawasaka mpaka mnawapata leo mshindwe kuwapata wanaokatisha maisha ya mama zetu vikongwe?, nafikiri inawezekana, elekezeni nguvu zenu huko, tumalize tatizo hili,” aliagiza Dkt. Balele.
Aidha kwa upande mwingine amelitaka jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kushirikiana kwa karibu zaidi na viongozi wa sungusungu kwa kuhakikisha wanakuwa na mawasiliano ya karibu zaidi mara kwa mara ili kuwezesha kudhibiti vitendo vya uhalifu katika mkoa wa Shinyanga hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, 2010.

Post a Comment