Profesa Benno Ndulu. |
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli leo hii amemteua Profesa Florenss Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania badala ya Profesa Benno Ndulu ambaye ameombwa kukabidhi ofisi haraka.
Rais Dk John Magufuli amteua Profesa Florens Luoga kuwa Gavana wa
Benki Kuu Tanzania. Amtaka Gavana wa sasa Beno Ndulu kuanza utaratibu wa
kukabidhi ofisi haraka.
Rais Magufuli alifanya uteuzi huo wakati wakati wa kutunuku vyeti vya
pongezi maalum wajumbe wote waliohusika kuchunguza kiwango, aina na
thamani ya madini katika makinikia.
Kabla ya uteuzi huo, Profesa Luoga alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA). Akihutubia Taifa
baada ya kuwatunuku wajumbe hao, Rais Magufuli amewaonya watu
wanaopotosha takwimu rasmi za serikali na kutoa za uongo.
Kutokana na tabia hiyo ya baadhi ya watu, Rais amemwagiza Waziri wa
Katiba pamoja na vyombo vya dola kuwachukulia hatua watu wanaopotosha
takwimu wakati ukweli wanaujua.
"Vita ya kupigania rasilimali za nchi ni ngumu sana, ninapata shida
kubwa kutokana na kuongoza vita hii, inaniumiza sana lakini nimetumwa na
Watanzania kuifanya kazi hii kwa moyo wangu wote"
Rais Dk John Magufuli
Rais Magufuli amewashutumu watu wanaopinga juhudi za serikali za
kutetea rasilimali za nchi akisema wanapigania matumbo yao "Wanaopinga
juhudi za serikali za kupigania rasilimali za nchi wanatetea pesa
walizoahidiwa na wezi wa rasilimali zetu" Rais Dk John Magufuli, Ikulu,
Dar es Salaam.
Rais Magufuli ashukuru vyama vya upinzani kwa kuruhusu wanachama wao
kuwepo katika kamati za madini kwa sababu maendeleo hayana vyama. Asema
fedha zikiongezeka hata ruzuku za vyama zitaongezeka.
Post a Comment