Russia imemfukuza nchini
wakala wa kijasusi aliyekuwa akifanya kazi kwa ajili ya mashirika ya kijasusi
ya Marekani na Latvia kwa wakati mmoja kwa zaidi ya miongo miwili.
Mtu huyo alikuwa akikusanya
taarifa za kijeshi kwa ajili ya mashirika ya kijasusi ya Marekani na Latvia.
Shirika la Ujasusi la Russia
limemtaja Andrejs Dudarevs inspekta wa ngazi ya juu wa shirika la anga la
Latvia kama wakala wa kijasusi aliyekuwa akitumikia nchi mbili na hivyo kumpiga
marufuku kuingia Russia kwa miaka kumi.
Kanali ya habari ya Russia ya
NTV imetangaza kuwa Dudarevs aliyafanyia kazi mashirika ya kijasusi kwa muda wa
miaka 22, ambapo kwa mara ya kwanza aliifanyia ujasusi Latvia na kisha
Marekani, huku akizikusanyia nchi mbili hizo taarifa zinazoihusu Wizara ya
Ulinzi ya Russia.
Mwaka 2011 jasusi huyo
alijaribu kuwasiliana na idara za usalama za Russia na miaka mitatu baadaye,
alikutana na wawakilishi wa shirika la ujasusi la Russia akiomba kazi katika
sekta ya masuala ya anga ya kijeshi, mkabala na kuvujisha taarifa kuhusu
mawakala wenzake wa Magharibi na kwa ajili ya maslahi mengine ya kifedha.
Chanzo: Sauti
ya Radio Iran.
Post a Comment