Rais Joseph
Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo anatarajiwa kumteua Waziri Mkuu,
licha ya upinzani ambao ulipaswa kutoa jina hilo, kugawanyika, juu ya nani
atakayeteuliwa.
Mpaka sasa upinzani
umegawanyika pande mbili, ukiwemo ule unaopinga kuteuliwa kwa Felix Tshekedi
licha ya kuongoza kundi kubwa na upande mwingine ni wanaomuunga aliyekuwa
mshauri mkuu wa marehemu Tsichekedi ambaye alifukuzwa kwenye chama hicho, baada
ya kufanya mazungumzo na Rais Kabila.
Hata hivyo kwa
mujibu wa rais kabila, kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya ni kutatatua mvutano
uliozuka, kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya tarehe 31 Desemba mwaka jana,
makubaliano ambayo yanataka waziri mkuu atoke upande wa Muungano wa upinzani.
Lakini hadi
sasa bado hawajaafikiana kuhusu namna ya kufanya uteuzi, kutokana na mgawanyiko
ulitokea upande huo wa upinzani baada ya kifo cha marehemu mkogwe wa upinzani
Etienne Tshisekedi, ambae alikuwa anaongoza muungano huo, licha mtoto wake
kuteuliwa kuchukuwa nafasi yake hiyo.
Aliyekuwa waziri Mkuu wa DRC, Samy Badibanga. |
Hatua hii inafuatia aliyekuwa waziri mkuu
katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Samy Badibanga kujiuzulu kama sehemu ya makubaliano yaliyoongozwa na kanisa
katoliki kumaliza mzozo wa kisiasa nchini humo.
Kwa
upande wake Rais Joseph Kabila, aliwaambia wabunge wa nchi hiyo kuwa atamteua
waziri mkuu kutoka upinzani ndani ya saa 48 zinazokuja.
Bwana
Kabila alisema kuwa atafuata tararibu zilizoafikiwa kama sehemu ya makubaliano
na upinzani ambayo yanataka uchaguzi kuandaliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Chanzo: BBC Swahili News.
Post a Comment