Mmoja wa walimu wa shule ya msingi akiwa kazini. |
WALIMU wa sekondari hawana
mbinu za ufundishaji wa shule za msingi, hawakufundishwa saikolojia ya
kufundisha shule za msingi, Raia Mwema imeambiwa.
Pia imeelezwa kwamba mbinu za kuwaandaa walimu hutofautiana kutegemea ufundishaji wa shule za chekechea, msingi ama sekondari hivyo ni makosa kuchukua walimu wa sekondari kufundisha shule za msingi.
Maamuzi ya Serikali ya kuhamisha baadhi walimu wa sekondari kwenda kufundisha shule za msingi ili kukabiliana na upungufu yamepigwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa madai kuwa kwa mujibu wa sheria Serikali ilipaswa kufanya majadiliano na chama hicho.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako
Wiki iliyopita, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi Elimu ), Benard Makali aliiambia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) juu ya mpango wa Serikali wa kuwahamishia walimu wa sekondari wa masomo ya sanaa kwenda kufundisha shule za msingi.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu huyo, shule za msingi nchini zina upungufu wa walimu 47,151 wakati katika shule za sekondari kuna ziada ya walimu wa sanaa 7,463.
Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CWT, Ezekiah Oluoch ameliambia Raia Mwema ya kuwa walimu wa sekondari ni wachache kuliko serikali inavyosema na kwamba ni uamuzi wa makosa uliochukuliwa.
Chanzo: Raia Mwema
Post a Comment