Abraham Poincheval akiwa ameatamia mayai ya kuku.
Msanii kutoka Ufaransa Abraham Poincheval anaendelea kutamia mayai ya kuku akiwa na matumaini kwamba mwishowe yataangua vifaranga.


Msanii huyo anatumia joto kutoka kwa mwili wake kutamia mayao hayo 10.

Poincheval ambaye hufanya uigizaji wa kuigiza mambo ya ucheshi lakini ya hatari tayari ameishi wiki mbili ndani ya dubu, miongoni mwa mambo mengine ya kushangaza.

Moja katika vituko alivyowahi kufanya Abraham Poincheval
Atakuwa katika chumba maalum ambacho anatamia mayai, ambapo watalii wanaweza kumtazama katka makumbusho ya Palais de Tokyo mjini Paris.

Anatarajia kutamia mayai hayo kwa siku 21 hadi 26.
"Kusema mweli, kimsingi, ni kama nimekuwa kuku," anasema.

Badala ya kutamia mayai hayo kwa kuchutuma juu yake moja kwa moja, anatumia kiti maalum ambacho kina mfuko eneo lake la kukalia. Hapo ndipo mayai hayo yamewekwa.

Poincheval atakuwa amejifunga blanketi kuzuia joto kupotea.
Aidha, anapanga kula vyakula vinavyoongeza sana joto mwiliki, kama vile tangawizi.

Wakati wa haja, atatumia kijisanduku kidogo kilichomo mvunguni mwa kiti chake.

Ndipo mayai hayo yaangue vifaranga, hahitaji kuondoka zaidi ya dakika 30 kwa siku. Anapanga kutumia muda huo kula chakula.

Chanzo: BBC Swahili News.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top