Uwezo wa klabu ya Barcelona kumpatia Lionel
Messi kandarasi mpya yenye nyongeza ya mshahara itategemea uwezo wao wa kuvutia
mapato kutoka kwa wadhamini na uuzaji wa wachezaji ,amesema mkurugenzi mkuu wa
klabu hiyo Oscar Grau.
Kandarasi ya Messi inakamilika 2018 na
anatarajia kupewa mkataba mpya huku ikiripotiwa huenda akapewa kitita cha pauni
milioni 21 wanazopata Luis Suarez na Neymar.
''Tunahitaji wachezaji wazuri lakini pia lazima
kuwa na kipaumbele '',aliongezea.
La Liga huweka mkataba na kila klabu kuhusu
matumizi yao kila mwanzo wa msimu, ambapo huyazuia mabodi kutotumia zaidi ya
asilimia 70 ya bajeti yake ya mapato.
Kandarasi zenye mishahara mikubwa walizopatiwa
Suarez na Neymar ambazo zitakamilika 2021, huchukua kiwango kikubwa cha matumizi
ya timu hiyo.
Messi mwenye umri wa miaka 29, anaripotiwa
kupokea pauni milioni 19 na Grau anasema kuwa nyongeza yoyote lazima ifikiriwe
sana.
Chanzo: BBC
Swahili
Post a Comment