Kundi la askari wa Al-Shabab likiwa katika harakati zake |
Wapiganaji hao
wanadai kuwaua wanajeshi wengi kwenye shambulio hilo katika kambi ya Kulbiyow
kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa nchi hiyo na Kenya.
"Mujahideen
(wapiganaji) wawili walivurumisha magari yaliyokuwa na mabomu na kuyalipua
kwenye lango la kambi hiyo ya mji wa Kulbiyow kabla ya wapiganaji wengine
kuingia.
Baada ya makabiliano makali, tumefanikiwa kuiteka kambi," mmoja
wa wasemaji wa al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia shirika la habari
la Reuters.
Msemaji huyo
amedai kundi hilo limewaua wanajeshi zaidi ya 50 na kutwaa magari na silaha za
wanajeshi hao, taarifa ambazo msemaji wa majeshi ya Kenya amekanusha.
Kanali Paul
Njuguna ameambia Reuters: "Ni uongo. Operesheni ya kijeshi inaendelea.
Tunaendelea kupokea taarifa."
Al-Shabab wamekuwa
wakipigana dhidi ya serikali ya inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na
jamii ya kimataifa.
Ramani ikionesha maeneo yaliyokuwa chini ya Al-Shabab |
Wanajeshi wa Kenya pamoja na wanajeshi kutoka Djibouti, Uganda na Ethiopia, chini ya Amisom, wamekuwa wakisaidia serikali hiyo yenye makao yake Mogadishu.
Chanzo: BBC
News
Post a Comment