CHAMA Cha wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya
Tanzania (TUGHE) mkoani Shinyanga kimelalamikia kitendo cha baadhi ya waajiri
katika idara za serikali kuzuia kufanyika kwa vikao vya mabaraza ya wafanyakazi
kwa mujibu wa sheria.
Hali hiyo
imetajwa kushusha ari ya wafanyakazi kufanya kazi katika sehemu za kazi
kutokana na kukosa eneo la kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili na
kwamba moja ya kazi ya mabaraza ni kuishauri menejimenti juu ya mambo muhimu
yanayohusu maslahi ya wafanyakazi.
Akisoma
risala ya viongozi wa TUGHE juzi kwa katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga (RAS),
Abdul Dachi ambaye ndiye mwajiri mkuu wa watumishi wa serikali, katibu wa TUGHE
mkoani humo, Tabu Mambo alisema baadhi ya ofisi za serikali haziruhusu
kufanyika kwa vikao vya mabaraza ya wafanyakazi.
Akielekea katika ukumbi wa mikutano akiongozwa na mwenyekiti wa TUGHE mkoa. |
Alisema
kutofanyika kwa vikao hivyo kunawanyima haki wafanyakazi kufahamu bajeti ya
taasisi husika na hivyo kusababisha kuwepo kwa malalamiko wakati wa utekelezaji
wake pamoja na kwamba mabaraza hayo yameundwa kwa mujibu wa sheria.
Mambo
alifafanua baadhi ya changamoto zinazowakabili watumishi wa umma ni kima kidogo
cha mishahara ambacho hakikidhi mahitaji ya mwezi mzima ya mfanyakazi ikiwemo
makato makubwa ya kodi inayokatwa kila mwezi ambapo walishauri makato hayo
yapunguzwe.
Hapa ni wimbo wa Mshikamano (Solidarity) |
Hapa mgeni rasmi anaweka saini yake katika kitabu cha wageni. |
Kwa upande
wake mwenyekiti wa TUGHE mkoani Shinyanga, John Mfutakamba alimweleza katibu
tawala huyo kwamba pamoja na changamoto zinazowakabili watumishi wa umma
watahakikisha wanatimiza wajibu wao kikamilifu ili uchumi wa nchi usiporomoke.
Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa akitoa neno kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na viongozi wa matawi ya TUGHE Shinyanga |
Viongozi wa matawi ya TUGHE wakimsikiliza mgeni rasmi. |
“Mheshimiwa
mgeni rasmi, pamoja na changamoto ulizoelezwa hapa, lakini napenda
kukuhakikishia kwamba tutaendelea kuchapa kazi kwa bidii na uaminifu mkubwa
chini ya rais ajaye wa awamu ya tano atakayechaguliwa, maana sisi kama
watumishi wa umma tunaelewa dhamana tuliyonayo,”
“Dhamana ya
uchumi wa nchi imo mikononi mwetu, ni wazi tunapaswa kutimiza wajibu wetu
kikamilifu, tutakuwa makini katika maeneo yetu ya kazi na tunaamini
hatutazembea, lakini pia tutatumia vikao vyetu vya TUGHE katika kujadiliana juu
ya uboreshaji wa hali bora ya kazi katika maeneo yetu,” alieleza Mfutakamba.
Kwa upande
wake katibu tawala aliwahakikishia viongozi hao kwamba ofisi yake itajitahidi
kushughulikia changamoto zote zilizopo ili kuwawezesha wafanyakazi kufanya kazi
zao kwa hali ya amani na utulivu na kwamba maeneo yote yenye mabaraza ya
wafanyakazi vikao vyote vya kisheria vitakuwa vikifanyika.
Post a Comment