Edward Lowassa, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya CHADEMA (UKAWA) akiteta jambo na mmoja wa mama lishe wa Tandale. |
S. H. KOVA |
JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LAPIGA
MARUFUKU WAGOMBEA WA VYAMA VYA SIASA KUFANYA VITENDO VINAVYOHATARISHA USALAMA.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limegundua kwamba kuna baadhi ya wagombea wa vyama vya siasa ambao wameanziasha mtindo wa kutembelea maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam kama vile vituo vya daladala, masoko mbalimbali, n.k. kwa madai ya kuyatembelea makundi ya watu wenye kipato cha hali ya chini.
Kutokana na uzoefu uliojitokeza katika ziara hizo zisizo rasmi ni
kwamba imeonekana mikusanyiko mikubwa isiyotegemewa katika hali ambayo inaashiria
uvunjivu wa amani. Wakati wa ziara za aina hiyo yamejitokeza makundi ya watu mbalimbali
kama vile waendesha bodaboda, machinga na makundi mengine katika namna ambayo imeleta
taharuki pamoja na usumbufu unaotokana na makele, msongamano au shughuli za
usafiri kusimama kabisa.
Tarehe 25/08/2015 majira ya saa 12:00 mchana katika makutano ya mtaa wa
SWAHILI na UHURU Kamnda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Kamishna Msaidizi Mwandamizi
LUCAS MKONDYA alilazimika kukutana ana kwa ana na mgombea urais wa CHADEMA Mhe.
EDWARD LOWASA ili kumpa tahadhali hiyo ya kiusalama. Mgombea huyo alikuwa
amezungukwa na wapanda pikipiki wasiopungua arobaini pamoja na magari mengi
katika hali ambayo ilileta msongamano katika eneo hilo ya barabara za Swahili
na Uhuru.
Msongamano huo ulileta athari na malalamiko kutoka kwa watumiaji wengine
wa barabara jijini Dar es Salaam.
Aidha, imegundulika kwamba mgombea huyo alianzia kuzunguka maeneo
mbalimbali ya Temeke kuanzia tarehe 24/08/2015 akitumia vyombo mbalibali vya usafiri
ikiwemo mabasi ya abiria.
Ni lazima ieleweke wazi kwamba moja ya kazi za Jeshi la Polisi ni
kuthibiti makundi makubwa ya watu katika namna ambayo kiongozi yeyote wa aina
ya wagombea urais anatakiwa kulindwa katika kipindi chote cha kampeni hadi siku
ya uchaguzi n.k. Ni vyema wagombea mbalimbali hususani wagombea urais waonyeshe
ushirikiano wa hali ya juu kwa Jeshi la Polisi ili kuzuia madhara ya aina
yoyote dhidi yao. Hivyo, ni muhimu wakajihadhari kwenda katika makundi yasiyo
rasmi kwa sababu za kiusalama.
Tunawashauri viongozi wa vyama pamoja na wagombea wao wafuate ratiba za
kampeni za mgombea urais/mgombea mwenza kwa vyama vya siasa kama ilivyotolewa
na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuondoa hisia za kufanyika kampeni nje ya
ratiba.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA
POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
DAR ES SALAAM
Post a Comment