Rais Jakaya Kikwete na mwenyekiti wa Taifa wa CCM akimtambulisha rasmi Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM.
Waziri wa Ujenzi nchini Tanzania, John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Kagame siku ya Jumamosi, Julai 18 2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Magufuli baada ya kufungua rasmi michuano hiyo, atashuhudia mchezo wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya Kagame, mechi itakayowakutanisha miamba ya Afrika Mashariki timu ya Yanga dhidi ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya.

Michuano ya Kagame inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya jumamosi kwa michezo mitatu, ukindoa mecho ya Yanga Vs Gor Mahia, mechi zingine zitakua ni kati ya APR dhidi ya Al Shandy uwanja wa Taifa saa 8 mchana, KMKM Vs Telecom saa 10 jioni uwanja wa Karume.

Kuanzia leo tutakua tunawaleta kwa ufupi timu zinazoshiriki michuano hiyo mwaka huu, na kwa kuanza tunaanza na kundi A;

Mchezo wa ufunguzi kati ya Yanga dhidi ya Gor Mahia unaonekana kuteka hisia za wapenzi wa soka kwa ukanda wa Afrika Mashariki, kwani ni takribani miaka 19 timu hizo mbili haziwaji kukutana katika ardhi ya Tanzania.

Chanzo: MichuziBlog
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top