Rais
Jakaya Kikwete amesema idadi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kuwania urais ni
kubwa, hivyo ni lazima wawape viongozi muda wa kuwachuja lakini akawataka
wasiwanunie baada ya kufanya uamuzi.
Rais
Kikwete alisema hayo jana katika hotuba yake ya kuvunja Bunge ambayo iliibua
waziwazi ushabiki kwa wagombea, hasa baada ya kumtaja aliyekuwa waziri mkuu
wake wa kwanza, Edward Lowassa kwa ajili ya kumshukuru.
Akitoa
salamu zake kwa wagombea hao, Rais Kikwete aliwapongeza na kuwatakia mafanikio
mema katika safari yao.
“Wale
wanaogombea urais waliomo humu (bungeni) nawatakia kila la kheri na nawashukuru
kwa kuonyesha nia ya kunipokea mzigo huu mzito. Nawatakiwa heri katika
matamanio yenu,” alisema Rais Kikwete ambaye aliingia Ikulu mwaka 2005.
“Mko
wengi, wote ni vigogo na mmetupa kazi kama kamati kuwachuja kwa hiyo msitununie
tukifanya maamuzi.”
Lowassa afunika
Wakati
akihitimisha hotuba hiyo, Rais aliwashukuru watu mbalimbali waliofanya kazi
kwenye Serikali yake, lakini hali ilikuwa tofauti alipomtaja Lowassa ambaye
alifanya naye kazi kwa miaka miwili.
Alimshukuru
pia, Makamu wake, Dk Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na
baadaye wabunge na viongozi wengine.
Alianza
kwa kuwashukuru huku akiwataja majina. Kila alipotaja majina ya viongozi hao,
wabunge walipiga makofi kwa kugonga meza zao. Hata alipomtaja Dk Bilal na Pinda,
wabunge hao walishangilia kwa kawaida.
Hata
hivyo, alipofikia kutaja jina la Lowassa, kelele za wabunge zilikuwa maradufu,
wengi wao wakipiga meza kushangilia, hali iliyomfanya Rais Kikwete anyamaze kwa
sekunde kama 50 na ndipo Lowassa aliposimama na kuinamisha kichwa kuonyesha
kukubali shukrani hizo.
Wabunge
waliendelea kumshangilia hadi alipoketi na ndipo Rais Kikwete akaendelea kutoa
shukrani kabla ya kuhitimisha hotuba yake ya saa mbili na dakika 20.
Chanzo: Mwananchi
News
Post a Comment