Viongozi Kaskazini mwa Kenya wamesema kuwa
wapiganaji wa kundi la kigaidi kutoka Somalia la Al Shaabab waliuteka msikiti
mmoja katika kaunti ya Garissa kwa masaa kadhaa.
Wapiganaji hao waliwahutubia waumini waliokuwa
msikitini kwa karibu saa mbili kabla ya kutokomea mwituni.
Waliikosoa serikali ya Kenya na kuonya waumini
dhidi ya kuwa majasusi wa serikali ya Kenya.
Mwezi uliopita Al Shaabab walivamia chuo kikuu
cha Garissa na kuwaua watu 150 wengi wao wanafunzi.
Kundi hilo kutoka Somalia linaaminika kuwa na
wafuasi nchini Kenya ambapo limetekeleza mashambulizi kadha katika jitihada ya
kuilazimisha serikali ya Kenya kuondoa majeshi yake nchini Somalia.
Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa kikosi cha
kulinda amani cha muungano wa Afrika Amisom ambao wanaisaidia serikali dhaifu
ya Somalia kupigana na waasi wa Al Shabaab.
Source: BBC
Swahili News.
Post a Comment