WAZIRI wa Mambo ya ndani ya Kenya, Joseph Nkaissery: KATUUU!! HATUSALIMU AMRI!!! |
Nkaissery
alisema hayo jana katika Chuo Kikuu cha Garissa, kaskazini mwa nchi hiyo ikiwa
ni siku moja tu baada ya wanamgambo wa al Shabab kuvamia majengo ya chuo hicho,
kuua kigaidi wanafunzi 147 na kujeruhi makumi ya wengine katika chuo hicho.
Waziri
wa mambo ya Ndani wa Kenya ameongeza kuwa, serikali ya Kenya kamwe haitasalimu
amri mbele ya makundi hayo ya kigaidi ambayo yanafanya mauaji dhidi ya watu
wasio na hatia.
Akiashiria
juu ya azma ya serikali katika kukabiliana na makundi ya kigaidi, Joseph
Nkaissery amesema kuwa, maafisa usalama kwa kushirikiana na jeshi la Kenya
wanaendelea na operesheni kali dhidi ya wanachama wa kundi hilo la kigaidi.
Hii
ni katika hali ambayo Rais Hassan Sheikh Mohamoud wa Somalia ametoa mkono wa
pole kwa serikali na wananchi wa Kenya juu ya shambulizi hilo la kutisha nchini
Kenya, na amesisitizia udharura wa nchi yake na serikali ya Nairobi kuzidisha
ushirikiano wao wa kiusalama dhidi ya wanachama wa kundi hilo la kigaidi.
NCHINI
MISRI NAKO KUMEKUCHA!!! JESHI LATEKETEZA 100!!!
Watu
100 wameuawa katika mashambulizi makali ya anga ya yaliyofanywa na helikopta za
jeshi la Misri dhidi ya maeneo ya wanamgambo katika Peninsula ya Sinai
kaskazini mwa nchi hiyo.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo watu 100 wameuawa katika mashambulizi hayo yaliyofanywa
na helikopta aina ya Apache dhidi ya maeneo ya wanamgambo na kwamba makumi ya
wengine wamejeruhiwa vibaya.
Kabla
ya hapo, watu 40 waliripotiwa kuuawa katika mashambulizi hayo ya anga ya jeshi
la Misri.
Mashambulizi
hayo yamefanyika ikiwa ni siku moja baada ya watu wenye silaha kuvamia vituo
viwili vya upekuzi katika eneo hilo na kuua askari 15 wa nchi hiyo na
kujeruhiwa raia wengine wawili. Itakumbukwa kuwa tarehe 31 Januari mwaka huu,
Rais Abdel.
Source:
Radio Tehran
Post a Comment