Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM)

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Ngoyayi Lowassa.
BENDERA YA CHAMA CHA ACT.

VIONGOZI WA UKAWA KATIKA MOJA YA MIKUTANO YAO.



KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, OKTOBA 25, 2015 MENGI YAANZA KUNONG’ONWA!!!


WAKATI UMMA WA WATANZANIA UKITEGA MASIKIO KUSIKILIZA UTEUZI WA WAGOMBEA URAIS KUTOKA VYAMA MBALIMBALI VYA SIASA NCHINI, HUKU MVUTANO MKUBWA UKITARAJIWA KUWA KATI YA MGOMBEA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) NA YULE WA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA) MENGI YAANZA KUNONG'ONWA KWA CHINI CHINI.

MASIKIO YA WATANZANIA YAMETEGESHWA KWA HAMU KUSIKIA NI MGOMBEA YUPI ATAKAYETEULIWA NA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) ILI KUPAMBANA NA WAGOMBEA WENGINE KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI, IKIWEMO MUUNGANO WA VYAMA VYA CUF, CHADEMA, NLD NA NCCR-MAGEUZI (UKAWA).

HATA HIVYO KILA UPANDE KATI YA CCM NA UKAWA WANAKABILIWA NA HALI NGUMU YA KIMAAMUZI JUU YA MGOMBEA YUPI ANAYESTAHILI KUTEULIWA ILI KUWEZA KUKABILIANA NA USHINDANI MKUBWA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA HUU AMBAO HUENDA UKAANDIKA HISTORIA MPYA HAPA NCHINI.

PAMOJA NA VYAMA VYA NCCR, CUF, NLD NA CHADEMA KUUNGANISHA NGUVU ZAO KWA LENGO LA KUTAKA KUSIMAMISHA MGOMBEA MMOJA ATAKAYETOA UPINZANI WA DHATI, HATA HIVYO NGUVU HIZO ZINAWEZA KUATHIRIWA NA KUIBUKA GHAFLA KWA CHAMA CHA ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY (ACT-TANZANIA)  
  
CHAMA HICHO HIVI SASA KIMEANZA KUZOA KWA SEHEMU KUBWA MAMIA YA WANACHAMA KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI HUKU WALE WA CHADEMA WAKIONGOZA BAADA YA KUONGOZWA NA ZITO ZUBERI KABWE ALIYETIMULIWA HIVI KARIBUNI KUTOKA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)!!!

HATA HIVYO IPO MINONG’ONO ISIYO RASMI KWAMBA IWAPO CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KITAFANYA KOSA LA KIUFUNDI NA KUKATA JINA LA MMOJA WA WANACHAMA WAKE WANAOJIPANGA KUTAKA KUWANIA NAFASI HIYO MUHIMU YA KIUONGOZI HAPA NCHINI, WAZIRI MSTAAFU EDWARD NGOYAYI LOWASSA, HUENDA KIKAJIKUTA KIKIMPOTEZA KIONGOZI HUYO MAHIRI ANAYEHOFIWA KUKIMBILIA KATIKA CHAMA CHA ACT.

INAHISIWA IWAPO LOWASSA ATAJIUNGA NA CHAMA HICHO  ATAKABIDHIWA RASMI BENDERA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA TIKETI YA ACT AMBAPO INAELEZWA IWAPO ATASHINDA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, BASI WAZIRI MKUU WAKE WA KWANZA ATAKUWA BW. ZITTO ZUBERI KABWE.

WACHUNGUZI WA MASUALA YA KISIASA WANAAMINI KWAMBA IWAPO ITATOKEA LOWASSA KUKIMBILIA ACT, NI WAZI MNYUKANO MKALI KATIKA UCHAGUZI HUO WA OKTOBA 25, MWAKA HUU UTAKUWA KATI YA MGOMBEA HUYO NA MGOMBEA KUTOKA UKAWA, HUKU YULE WA CCM AKIBAKI KUWA MSINDIKIZAJI.

YAWEZEKANA IKAWA HIVYO NDIVYO, JAPO BADO NI MINONG’ONO TU ISIYO NA UKWELI WOWOTE, WACHA TUSUBIRI, MAANA WASWAHILI WALISEMA.

Lisemwalo Lipo, kama halipo basi lajaaaa!!!
Chaoooos!!!
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Asante kwa kutembelea mtandao huu

Post a Comment

 
Top