Viongozi wakuu wa vyama vikuu vya upinzani UKAWA wakiwasili makao makuu ya CUF kwa ajili ya kuzungumza na wanahabari leo |
Hatimaye viongozi wa vyama
vikuu vya upinzani vinavyounda UKAWA wameibuka
upya na kutangaza rasmi kutokuwa na imani na Tume ya Taifa ya uchaguzi
nchini kwa kudai kuwa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inaitumia tume hiyo
kutaka kusogeza uchaguzi mbele kwa lengo la kujiongezea muda wa kutawala.
Akisoma maadhimio ya
umoja huo baada ya kukutana ndani ya siku mbli jijini Dar es salaam mwenyekiti
mwenza wa umoja huo ambaye ni mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi mh JAMES
MBATIA amesema kuwa kutokana na hali ya hewa inayoendelea kuhusu sintofahamu ya
daftari la kupiga kura ni wazi kuwa sasa umoja wao hauna inami hata kidogo na Tume
ya Uchaguzi kwani imeonyesha wazi kuwa inashirikiana na serikali ya chama cha
mapinduzi kutaka kuhujumu uchaguzi ujao na kisha kuongeza muda wa uongozi wa
serikali hiyo kwa kisingizio cha kutokumalizika kwa uandikishwaji wa daftari la
kudumu la wapiga kura.
Amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi hadi sasa ikiwa imesalia takribani miezi mitatu pekee kuanza
kwa kampeni rasmi za uchaguzi haijaanza wala hakuna dalili za maandalizi yoyote
ya kufanyika kwa uchaguzi huo jambo ambalo linazidi kuleta wasiwasi kwa
watanzania na kuamini kuwa kuna njama za kuahirisha uchaguzi huo kama ilivyofanyika
kwa daftari la kudumu la wapiga kura.
“Kuna jambo
linashangaza sana, hadi sasa hakuna maandalizi yoyote yanayoashiria kuwepo kwa
uchaguzi huo ilihali imebaki miezi sita tu kufanyika kwa uchaguzi huo, hakuna
utaratibu wa vifaa vya uchaguzi huo, ambapo miaka iliyopita imekuwa ikifanyika
maadalizi mwaka mmoja kabla lakini uchaguzi huu hadi leo hakuna maandalizi ya
kuonyesha kuwa uchaguzi huo upo japo kuwa mwenyekiti wa tume hiyo anazidi
kuwadanganya watanzania kuwa uchaguzi huo upo,” alisema Mbatia.
Naye mwenyekiti wa
CHADEMA Freeman Mbowe amesema kuwa hakuna njia yoyote ya kuzia mabadiliko
ambayo yanataka kufanywa na ukawa kwa sasa hivyo tume hiyo isikubali kutumika
na serikali na badala yake ni lazima uchaguzi ufanyike mwaka huu kwa njiia
yoyote.
Source: Habari24 Blog.
Post a Comment