IWAPO
KATIBA INAYOPENDEKEZWA ITAKUBALIWA KAMA ILIVYO, BUNGE LA TANZANIA SASA LITAKUWA
HALINA MENO TENA KAMA LILIVYO HIVI SASA, JE, NI SAWA KUIPIGIA KURA YA HAPANA??? SOMA
VIFUNGU HIVI:-
Mipaka ya
bunge katika (Kama ilivyo ndani ya
katiba inayopendekezwa)
kutumia
madaraka yake;
132 – (1) Katika kutekeleza madaraka ya
kuisimamia serikali kwa mujibu wa katiba hii, wajibu wa bunge utakuwa ni kuishauri serikali
na endapo Bunge halitaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali katika
utekelezaji wa suala lililotolewa ushauri, basi Bunge litakuwa na haki ya
kuiwajibisha serikali kwa mujibu wa
madaraka lililopewa katika katiba hii.
(LAKINI SOMA KWA MAKINI KIFUNGU HIKI KINACHOFUATA):-
(2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1), Bunge
halitachukua hatua yoyote ya kiutendaji ambayo, kwa desturi ni shughuli za
serikali, na halitatoa maagizo yoyote ya kiutendaji kwa serikali na watumishi
wa umma: isipokuwa kwamba; Bunge litashauri kuhusu suala lolote lililo katika
dhamana ya waziri anayehusika.
LINGANISHA NA KATIBA YA SASA YA MWAKA 1977
KUHUSU IBARA HIYO IBARA YA 63 KIFUNGU KIDOGO (2) KINASOMEKA:
63. (2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho
chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya
wananchi, kuisimamia na kuishauri serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo
vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba
hii.
TAFAKARI!!!!
Post a Comment