RAIS WA RWANDA - PAUL KAGAME (kulia) AKILAKIWA NA RAIS JAKAYA KIKWETE. |
Wafuasi
wa chama tawala cha nchini Rwanda FDR wametaka Rais wa nchi hiyo Paul Kagame
agombee tena urais kwa muhula wa tatu.
Jumatatu
ya leo tarehe 6 Aprili ni siku ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya kimbari ya
mwaka 1994 huko Rwanda. Sambamba na siku hii, wafuasi wa chama tawala nchini
Rwanda wamechunguza hali ya kisiasa na kiuchumi ya nchi hiyo na kusema kuwa
kubakia madarakani Rais Paul Kagame kwa muhula mwingine wa tatu kutazuia
kuibuka mivutano na machafuko nchini Rwanda.
Waungaji mkono wa Rais wa Rwanda wanaamini kuwa mabadiliko makubwa yamejiri nchini humo katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Uchaguzi
wa Rais wa Rwanda unatarajiwa kufanyika mwaka 2017 na ili Kagame aweze kugombea
tena urais, katiba ya nchi hiyo itapasa kufanyiwa marekebisho.
Source:
Radio Iran
Post a Comment