WAUMINI WA KIISLAMU KATIKA MOJA YA IBADA ZAO |
WATOTO wengine 147 wamekutwa wakiwa wamehifadhiwa katika misikiti mitatu,
tofauti, wilayani Hai ikiwa ni siku chache tangu watoto wengine 29 wakutwe
wamefichwa mafichoni jirani na Manispaa ya Moshi na Lyamungo Wilaya ya
Hai.
Watoto hao wa kiume wenye umri kati ya miaka 10-21 waligundulika kufichwa
kwenye misikiti hiyo baada ya taarifa kutolewa za siri kwenye kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Wilaya ya Hai.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika watoto hao walipatikana kutokana operesheni iliyoendeshwa na kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo Machi 25 hadi 27 baada ya kupata taarifa.
Watoto hao wanadaiwa kutoka mikoa mbalimbali ambapo wanadaiwa kwamba walikuwa wakipatiwa mafunzo ya dini ya Kiislamu.
Misikiti ambayo watoto hao walikutwa ni Masjid Bilal uliopo Mtaa wa Kibaoni,ambako walikutwa vijana 70, Masjid Othman uliopo Mtaa wa Uzunguni walikutwa Vijana 50 na Msikiti wa kwa Kiriwe ambako walikutwa vijana
27.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro zinasema watoto hao walibainika kuishi na kulala ndani ya misikiti hiyo kwa madai ya kupewa mafunzo ya imani ya dini ya Kiislamu. Taarifa hizo zilieleza kuwa vituo hivyo havitambuliki kisheria.
Baadhi ya watoto waliohojiwa na makachero alikiri kukatishwa masomo katika shule walizokuwa wanasoma. Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo imeagizwa kufungwa kwa vituo hivyo ili watoto hao warejeshwe kwao.
“Hatua ya kwanza iliyochukuliwa baada ya kupatikana kwa watoto hao ni kufungwa kwa vituo kwa maana ya mafunzo kusitishwa hadi watakapofuata taratibu,” alisema.
Akizungumzia sakata hilo,Mkuu wa Wilaya ya Hai, Anthony Mtaka, alikiri kukutwa kwa vijana katika misikiti hiyo,ambao walikuwa wanajifunza mafunzo ya dini na kwamba baadhi yao walikatisha masomo.
Mtaka ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama katika Wilaya hiyo,alisema vijana hao baada ya kuhojiwa walieleza kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Morogoro, Singida, Tanga, Pwani na Dar es
Salaam.
Mach 8, mwaka huu watoto 18, wa jinsia tofauti wenye umri katika ya miaka miwili hadi 16, walikutwa wamehifadhiwa katika nyumba moja kata ya Pasua mkoani hapa na kuibua tafrani kubwa kwa wananchi wa Manispaa ya Moshi.
Mbali na watoto hao pia watoto wengine 11 wa kike wenye umri kati ya miaka 14 hadi 17, walikutwa wamehifadhiwa katika nyumba moja eneo la Lyamungo Wilaya ya Hai,Machi 11, hali ambayo imeanza kuibua wasiwasi mkubwa kwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Source: Majira News Paper
Post a Comment