Saudi Arabia imekatalia mbali tumbili wanne
kutoka Sweden kufuatia tofauti za kidiplomasia.
Tumbili hao wanne ambao ni kutoka jamii ya
Amazonia ya tumbili wadogo zaidi duniani walikuwa msaada kutoka hifadhi ya
wanyama ya Skansen iliyoko Stockholm.
Afisa mkuu wa hifadhi hiyo Jonas Wahlstrom
anasema kuwa tumbili hao walikuwa wanapaswa kupelekwa katika hifadhi ya wanyama
ya Riyadh.
"hawataki
tumbili hao tena kufuatia utata uliopo wa kisiasa'' alisema Wahlstrom.
Mwezi uliopita
Saudi Arabia ilimuondoa balozi wake huko Sweden baada ya taifa hilo la bara
Uropa kukatiza mkataba wa uuzaji wa silaha kwa himaya hiyo.
Tumbili hao
wanauzani mdogo sana wa takriban gramu 100 pekee.
Saudia ilimzuia
balozi wa Sweden kuhutubia umoja wa mataifa ya kiarabu
Mwezi uliopita
Saudi Arabia ilimzomea waziri wa maswala ya kigeni wa Sweden Margot Wallstrom
kwa kuingilia maswala ya ndani ya Saudia.
Saudi Arabia
ilikasirishwa sana na matamshi ya balozi huyo hadi ikapiga turufu na kumzuia
kuzungumza katika jumuia ya Waarab huko Cairo.
VATICAN
NAKO KWAFUKUTA:
Mzozo wa kidiplomasia umezuka kati ya makao
makuu ya papa mtakatifu ya the Vatican na Ufaransa kuhusiana na uteuzi wa
balozi mpya wa Ufaransa, mjini Rome.
Rais wa Ufaransa Francois Holland,
amempendekeza muumini mmoja wa kanisa hilo ambaye ni mpenzi wa jinsia moja kuwa
balozi wake mjini Vatican.
Lakini utawala wa Vatican umesema uteuzi huo
haukubaliki.
Makao makuu ya papa mjini The Vatican
hayajasema lolote kuhusiana na uteuzi huo, lakini ni dhahiri kuwa baadhi ya
maafisa wakuu katika kanisa hilo hawajakubali msimamo wa papa kuhusiana na waumini
wa kanisa hilo ambao ni wapenzi wa jinsia moja.
Papa alinukuliwa akihoji kuwa yeye hawezi
kumhukumu mtu yeyote kwa misingi yoyote.
Serikali ya Ufaransa ilimteua laurent Stefanini
kuwa balozi wake mjini vatican mnamo mwezi Januari mwaka huu.
Balozi Stefanini mwenye umri wa miaka
55, amekiri hadharani kuwa yeye anashabikia mapenzi ya jinsia moja na amewahi
kufanya kazi katika ubalozi huo mjini Roma na amekuwa mshauri wa masuala ya
kidini katika wizara ya mambo ya nje ya ufaransa.
Kwa sasa hakuna upande unaoonekana kuwa tayari
kubadili msimamo wake.
Ufaransa ilhalalisha ndoa za jinsia moja mwaka
2013 na uamuzi wa The vatican wa kukataa kumkubali balozi Stefanini huenda
ikawa ni thibitisho la The vatican la kutoidhinisha msimamo huo wa Ufaransa.
Source: BBC
Swahili
Post a Comment