Muungano wa mashirika ya haki za binaadamu
nchini Kodivaa yameingiwa na wasiwasi juu ya nchi hiyo kutuma askari wake
kwenda kuungana na vikosi vya nchi nyengine za magharibi mwa Afrika kupambana
na kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram nchini Nigeria.
Muungano huo ulitangaza kuwa badala ya serikali ya Yamoussoukro kutuma askari
wake kupambana na kundi hilo, inatakiwa kujikita katika kudhamini usalama na amani
kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.
Aidha muungano huo umesisitiza kuwa, wananchi
wa Ivory Coast wana wasiwasi kwamba, hali inaweza kuwa tete kiusalama na
kisiasa ikiwa askari wa nchi hiyo watatumwa kupambana na Boko Haram.
Umeongeza kuwa, wanakubaliana na suala la
kupambana na wanamgambo wa kundi hilo, lakini hali inayotawala kwa sasa Kodivaa
hairuhusu kujiingiza katika vita vingine.
Mwezi uliopita Rais Alassane Ouattara
alitangaza azma ya nchi yake kutuma askari wake mwezi huu wa Aprili kwa ajili
ya kujiunga na muungano wa kieneo unaopambana na Boko Haram.
Source: Radio
Tehran
Post a Comment