Kwa
mara ya kwanza Ethiopia imeteketeza tani 6.1 za pembe za ndovu na bidhaa zake
kwenye hafla iliyoandaliwa Ijumaa katika bustani ya Gulele katika mji mkuu
Addis Ababa.
Pembe
hizo pamoja na bidhaa zingine za pembe za ndovu zilikamatwa zaidi ya miaka 30
iliyopita katika maeneo mbalimbali nchini humo na pia zikisafirishwa kwenye
uwanja wa kimataifa wa ndege wa Bole.
Naibu
waziri mkuu wa Ethiopia Demeke Mekonnen amesema kuteketezwa kwa pembe hizo ni
hatua ya nchi yake ya kuhifadhi na kulinda raslimali zake asili pamoja na
wanyama pori kwa ajili ya maendeleo endelevu.
Demeke
amesisitiza haja ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa kukabiliana
na tatizo la ujangili na biashara haramu ya wanyamapori.
Mkurugenzi
wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP nchini humo bwana
Samuel Bwalya amesema uharibifu huo wa pembe za ndovu inaonyesha dhamira ya
Ethiopia ya kulinda rasilimali za wanyamapori na kupambana na biashara haramu
ya wanyamapori.
Source:
China Swahili Radio.
Post a Comment